Shuhudia hapa Waziri Nape Nnauye Alivyotembelea Kundi la Wasafi Classic Linaloongozwa na Diamond PlatinumzWaziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mheshimiwa Nape Nnauye ametembelea ofisi za Kundi la musiki wa kizazi kipya la Wasafi.

Pamoja na mambo mengine uongozi wa kundi hilo umemuomba waziri huyo kushughulikia changamoto mbalimbali zinazowakabili ikiwa ni pamoja na kupunjwa mapato yatokanayo na miito ya simu (Caller tunes), wizi wa kazi za wasanii, kupata eneo (Ukumbi wa Kisasa) kwa ajili ya kufanyia maonesho makubwa ya musiki, wasanii kupata elimu juu ya kulipa kodi kwa kazi zao na kuongeza kiwango cha uwiyano kwa nyimbo za kitanzania zinazopigwa redioni dhidi ya nyimbo za kigeni.

Kwa upande wake Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye  amehaidi kuzifanyia kazi changamoto hizo na kuifanya tasnia ya muziki kuwa ajira kubwa kwa vijana wengi kwa kuongeza vipato vyao na pato la taifa kwa ujumla.

“Nimewaahidi kuzifanyia kazi changamoto hizi mapema iwezekanavyo ili kuongeza kipato kwa wasanii hapa nchini,” amesema Mheshimiwa Nnauye.

Wasafi Classic ni kundi la Muziki wa kizazi kipya(Bongo Flavour) Tanzania linalomilikiwa na Msanii Naseeb Abdul (Diamond Platinumz) na mpaka sasa lina wasanii wapatao 16 na linaongozwa na mameneja Babu Tale, Said Fella na Sallam SK.


Kujua Mbinu Za Kumfikisha Kileleni Mwanamke Kwa Haraka: BONYZA HPA CHNI

Kujua Sehemu 10 Zinazompa Raha mwanamke wakati wa Tendo, BONYZA HAP 1UU
BOFYA LIKE KUUNGANA NASI FACEBOOK!During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip.
© Copyright Masama Blog | Designed By MASAMA TEAM
Back To Top