Shuhudia hapa Mwili wa kichanga cha siku moja ulivyookotwa Jijini Mwanza | Masama Blog


Shuhudia hapa Mwili wa kichanga cha siku moja ulivyookotwa Jijini Mwanza

Mtoto mchanga wa kiume anayekadiriwa kuwa na umri wa siku moja Jijini Mwanza amekutwa ametelekezwa kwenye makazi ya watu na mtu asiyefahamika baada ya kujifungua.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa mwanza, Ahmed Msangi

Tukio hilo limetokea katika  mtaa wa Medical Kata ya Kitangiri ilemela jijini Mwanza  na  mwili wa kichanga hicho umegunduliwa na watoto baada ya kuona kichwa kikiwa nje ya mfuko aina ya  lambo damu zikitoka.

Mwenyekiti wa Mtaa huo Bw Patrober Maginga akiwa eneo la tukio amelaani kitendo hicho cha kikatili na kwamba uongozi wa mtaa kwa kushirikiana wananchi watafanya uchunguzi kumbaini  mhusika wa tukio hilo na kumfikisha kwenye vyombo vya sheria.

Aidha Jeshi la Polisi kituo cha Kirumba  Jijini humo wamefika eneo la tukio na kuuchukua mwili wa kichanga hicho kwa uchunguzi na hatua zaidi.

BOFYA LIKE KUUNGANA NASI FACEBOOK!


UNAIJUA BIASHARA YA FOREVER LIVING?....Kama una mtaji kuanzia 250,000 hadi 1,020,000 na unapenda kujikwamua na kubadilisha maisha yako kupitia biashara hii Tupigie simu nambari 0625539100 au 0625539200