Serikali yafunguka kuhusu fao la kujitoa..Msikie Hapa WaziriWaziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi Ajira na Vijana) Bibi Jenista Mhagama amesema serikali itakaa na wadau ili kuangalia namna ya kulimaliza sakata la fao la kujitoa katika mifuko ya hifadhi ya jamii.

Waziri Mhagama ametoa kauli hiyo jana  katika mkutano wa sita wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) mjini Dodoma uliofunguliwa leo na Waziri Mkuu Mjini Dodoma, ambapo katika risala yake, TUCTA ilihoji kuhusu  marekebisho ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii na ucheleweshwaji wa malipo ya pensheni.

Mhagama alisema kuwa baada ya uongozi wa TUCTA kukamilika, itabidi wakutane na kukaa pamoja kuainisha sera inataka nini na hali ya uchumi ya sasa ikoje huku wakiangalia dhana nzima ya hifadhi ya jamii nayo inataka nini.

“Kuna haja ya kuangalia sera inataka nini, tunapaswa tuangalie mabadiliko ya kiuchumi katika nchi yetu na kutazama dhana nzima ya hifadhi ya jamii kwenye maisha yetu ya uzeeni. Tukikaa pamoja, yaani, mwajiri, mfanyakazi na Serikali, tutapata njia ya kisheria ya kuweza kulifunga jambo hili ili lisiendelee kuwa kero kwa wafanyakazi wetu,”alisema.

Msikilize hapa waziri Mhagama akifunguka.


Kujua Mbinu Za Kumfikisha Kileleni Mwanamke Kwa Haraka: BONYZA HPA CHNI

Kujua Sehemu 10 Zinazompa Raha mwanamke wakati wa Tendo, BONYZA HAP 1UU
BOFYA LIKE KUUNGANA NASI FACEBOOK!During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip.
© Copyright Masama Blog | Designed By MASAMA TEAM
Back To Top