Ticker

10/recent/ticker-posts

SABABU 10 ZINAZOWEZA KUSABABISHA MAPENZI KUPUNGUA/KUISHA

Image result for MREMBOMapenzi ni kitu Fulani tofauti sana kwenye hii dunia na hata nje ya hii sayari. Mapenzi kwa kiasi kikubwa sana yanasababisha hata mambo mengine kwenye hii 
dunia yaende sawa au yaende tofauti hata kama hayahusiani na mahusiano ya mapenzi. Vifo vingi hutokana na mapenzi, kuna magonjwa watu wanaumwa kisa mapenzi, kuna mambo watu wanayafanya si ya kawaida kisa mapenzi.



Ukiachilia mbali PESA, Mapenzi huwa yana nafasi kubwa sana kwenye kitu chochote ndani yahii dunia tunayoishi. Si masikini wala si tajiri, wote kwa pamoja wanahitaji mapenzi kutoka kwa wanaowapenda ili dunia iweze kwenda sawa kwa upande wao. Na ndio sababu hata mimi hapa ninaandika kuhusu mapenzi kwa sababu yananigusa hata mimi na hata wewe unayesoma hapa sasa.


Ukipata mpenzi anayekuelewa na kukupenda basi hata dunia iwe ya tabu vipi kwako utaiona inazunguka kama kawaida na maisha yatasonga mbele kwako kwa raha mustarehe, na hata matatizo mengine makubwa kwako huwa madogo kwa sababu tu unapenda na kupendwa kwa dhati.


Lakini ukiumizwa kwenye mapenzi au kutojaliwa kama wewe unavyojali basi hata dunia iwe na raha gani kwako utaiona chungu na hata raha ya maisha hutakuwa nayo hata kama una hela kiasi gani na hata kama una cheo kikubwa kama mfalme au hata rais. Wengine hufikia hatu ya kuteseka tu bila kuondoka kwenye mahusiano kwa kuogopa kuumizwa tena huko waendapo na wengine huondoka baadae sana wakiwa tayari wameshachelewa.


Kuna Sababu Nyingi Sana zinazoweza kusababisha mapenzi kupungua kwenye mahusiano yenu na wakati mwingine hata kusababisha kuachana. Mojawapo kati ya sababu hizo ni pamoja na hizi zifuatazo;-
1.       UONGO.
Hakuna kitu kibaya kama uongo kwenye mapenzi, uongo wa aina yoyote ile si mzuri kwa wanaopendana kwa dhati kwa sababu huweza kupunguza mapenzi na uaminifu kwa kiasi kikubwa sana miongoni mwa wanaopendana