OMMY DIMPOZ ATOA SABABU YA KUFANYA COLLABO TENA NA ALI KIBA ‘KAJIANDAE’ | Masama Blog


OMMY DIMPOZ ATOA SABABU YA KUFANYA COLLABO TENA NA ALI KIBA ‘KAJIANDAE’

Msanii wa bongo fleva, Ommy Dimpoz ambaye kwa sasa amerudi kwenye game na kolabo ya wimbo wa ‘Kajiandae’ aliyofanya na Ali kiba tena, ametoa sababu ya kuamua kufanya tena kollabo na msanii huyo.Ommy Dimpoz na AliKibaAkizungumza kwenye FNL ya East Africa Television, Ommy Dimpoz amesema mara ya kwanza alivyofanya kollabo ya Nai Nai na Alikiba ilikuwa ili atoke kimuziki, lakini kollabo ya sasa ni kama tu collabo zingine, na sio kumtumia kurudi kwenye game.“Nai nai ilikuwa mimi nimemshirikisha Ali, nilikuwa natafuta njia ya kuuona ugali, lakini sasa hivi tumekuja kama Ali na Ommy kazi ya pamoja, mimi nilikuwa zangu break, nimerudi kwa hiyo haijalishi nimeimba na nani”, alisema Ommy Dimpoz.Ommy Dimpoz alishawahi kumshirikisha Alikiba kwenye wimbo wa ‘Nai nai’ ambao ndio ulimtambulisha kwenye ulimwengu wa bongo fleva, na sasa kaamua kurudi na kazi nyingine akiwa na alikiba pia, inayoitwa ‘Kajiandae’.

BOFYA LIKE KUUNGANA NASI FACEBOOK!


UNAIJUA BIASHARA YA FOREVER LIVING?....Kama una mtaji kuanzia 250,000 hadi 1,020,000 na unapenda kujikwamua na kubadilisha maisha yako kupitia biashara hii Tupigie simu nambari 0625539100 au 0625539200