Nilipumzika Muziki Kula Bata – Ommy Dimpoz | Masama Blog


Nilipumzika Muziki Kula Bata – Ommy Dimpoz


Ommy Dimpoz akiwa na Rooney Visiwani humo
Akizungumza kwenye FNL ya East Africa Television, Ommy Dimpoz amesema watanzania wamekuwa na mtazamo tofauti sana hasa pale msanii anapokuwa kimya kwenye kazi zake, na kukimbilia kumlaumu.
“Mimi nilikuwa kimya nilikuwa nafanya mambo yangu mengine, lakini sio kama kukaa kwangu kimya nilikuwa nimepotea nimepotea kwenye muziki, unajua watanzania wamekuwa na tafsiri tofauti, kuna watu wanatake break kija Justin Timberlake wanakaa miaka 7 7, na mimi nilikuwa zangu vacation, ma Ibiza huko (Ibiza ni sehemu ambayo watu wenye mkwanja mrefu duniani ndio huenda kula bata), sasa nimerudi nataka kufanya kazi”, alisema Ommy Dimpoz.
Ommy Dimpoz ambaye amerudi na ngoma mpya ya Kajiandae ambayo amefanya na Alikiba na tayari ameshaachia video yake, imepata ushabiki mkubwa mitandaoni kutokana na video yake.
Msani Ommy Dimpoz amesahihisha mashabiki walipokuwa wakisema msanii huyo kafulia baada ya kukaa kimya muda mrefu kwenye game, na kusema aliamu tu kupumizka kwa muda na si kama alifulia.

BOFYA LIKE KUUNGANA NASI FACEBOOK!


UNAIJUA BIASHARA YA FOREVER LIVING?....Kama una mtaji kuanzia 250,000 hadi 1,020,000 na unapenda kujikwamua na kubadilisha maisha yako kupitia biashara hii Tupigie simu nambari 0625539100 au 0625539200