NAHREEL AFUNGUKA HAYA KUHUSU KUMFUKUZA SELLINE KATIKA LEBO YA THE INDUSTRY | Masama Blog


NAHREEL AFUNGUKA HAYA KUHUSU KUMFUKUZA SELLINE KATIKA LEBO YA THE INDUSTRY

Story zilianza kuvuma mitandaoni zikimuhusisha chipukizi ambaye alikuwa chini ya lebo ya muziki ya The Industry (Selline) na uongozi wa lebo hiyo kuwa uongozi huo umemtema mwanadada huyo katika lebo hiyo.
Kuondoa utata wa mambo Peimemtafuta C.E.O wa lebo hiyo Nahreel na kupiga nae story kuhusiana na suala hilo, Nahreel amefunguka juu ya hilo na kuthibitisha kuwa habari hizo zina ukweli na wamefanya hivyo kutokana na utovu wa nidhamu wa msanii huyo.
“Yes, tumemsimamisha msanii wetu mmoja ambaye anaitwa Selline, na ni kwasababu tu ya utovu wa Nidhamu na kushindwa kufanya kazi chini ya uongozi. Mambo mengi ni ngumu kuelezea kwenye media lakini kiufupi ni hivyo tu. Kwahiyo sasa hvi kazi yoyote inayomuhusu msanii huyo sisi hatuhusiki nayo.”Alisema Nahreel.
Unaweza kumsikiliza Nahreel akibonga juu ya hilo kwa kuplay hii video hapa chini.

BOFYA LIKE KUUNGANA NASI FACEBOOK!


UNAIJUA BIASHARA YA FOREVER LIVING?....Kama una mtaji kuanzia 250,000 hadi 1,020,000 na unapenda kujikwamua na kubadilisha maisha yako kupitia biashara hii Tupigie simu nambari 0625539100 au 0625539200