MWANAMUME mmoja wa miaka 40 amelazwa katika hospitali kuu ya Murang’a baada ya kushambuliwa na mkewe kwenye sehemu nyeti zake hapo Jumapili jioni.

Polisi walimtambua baba huyo wa watoto wawili kama Bw John Njoroge Maina kutoka kijiji cha Kambirwa eneo bunge la Kiharu.

Akiongea na polisi akiwa kwenye wadi, mwanamume huyo alifichua kuwa mkewe alimshambulia kwa makucha na kujaribu kunyofoa sehemu nyeti zake huku akimwacha na majeraha mabaya.

Ilibidi madaktari kumfanyia upasuaji wa dharura ambapo walishona uzazi wake ambao ulikuwa ukivuja damu.

Kulingana na Bw Maina, yeye na mkewe wa miaka 28 walianza mzozo saa tatu za usiku kuhusiana na tabia ya mwanamme huyo ya kulewa kila wakati.

“Nilikuwa naenda usingizi na nilikuwa nishavua nguo na nilipokuwa namsihi mke wangu twende kulala, alikamata sehemu nyeti zangu na kuzivuta kwa nguvu huku akizikata kwa makucha yake,” Bw Maina aliambia polisi hapo Jumanne.

Alipiga mayowe na majirani wakaja na kumkimbiza hospitali ambapo alifanyiwa upasuaji na sasa yuko hali salama.

Afisa mmoja wa polisi aliyemhoji alisema watamkamata mkewe na kumshtaki kwa kosa la kusababisha majeraha.

Mwanamme huyo aliambia polisi wamekuwa wakizozana na mkewe kila wakati kwa sababu yeye huwa na tabia ya kulewa.

Sumu
Tukio hili linakuja miezi mitano tu baada ya mwanamke mmoja kutoka Kaunti hiyo kufungwa jela miaka mitatu na mahakama ya Murang’a kwa kujaribu kumpa sumu mumewe na kumpiga.

Bi Purity Wanjiku Mbaruku ambaye ni mama wa watoto wanne alishtakiwa kwa makosa mawili mbele ya Hakimu Mkuu mkazi Bw Joseph Masiga.

Katika shtaka la kwanza, Bi Wanjiku alishtakiwa kuwa mnamo Agosti 24 mwaka huu katika kijiji cha Matongu, lokesheni ya Kimathi eneo la Kiharu, alijaribu kumpa sumu mumewe Bw Charles Mbaruku Kimani.Vile vile alishtakiwa kwa kumpiga na kumjeruhi mumewe.

Katika shtakaka la kwanza, kiongozi wa mashtaka Bw Paul Gathara alieleza mahakama kuwa mshtakiwa alimkaba koo mlalamishi na kujaribu kumnywesha dawa ya kuua kupe aina ya 'Tria-Tix’ usiku saa nne na nusu.

Alielezea mahakama kuwa Bi Wanjiku alikusudia kumuua Bw Kimani kwa kumpa sumu hiyo hatari.

BOFYA LIKE KUUNGANA NASI FACEBOOK!


Je wewe una mtaji wa Ths.250,000/= au 510,000 au 1,020,000?..na unahitaji kufanya biashara kubwa kwa mtaji huo ufanikiwe?..basi kama ndiyo njoo tukuonyesha njia ya kutekeleza malengo yako...piga 0625 539 100

 
Top