MWANA FA AFUNGUKA HAYA KUHUSU VIDEO YA “DUME SURUALI” | Masama Blog


MWANA FA AFUNGUKA HAYA KUHUSU VIDEO YA “DUME SURUALI”

Jana November 21 ndio siku ambayo iliachiwa audio ya wimbo mpya wa mkali wa Hiphop kutoka Bongo Tanzania Mwana FA “Dume Suruali” ambao kafanya na mwanadada Vanessa Mdee.
Kwenye kipindi cha XXL cha Clouds fm ndipo ngoma hiyo ilizinduliwa rasmi na mwanadada Vanessa Mdeeakatusanua kuwa kichupa cha ngoma hiyo kitaachiwa rasmi leo katika mitandao ikiwa ni tayari imekwisha wasilishwa katika vituo mbali mbali vya Televisheni ikiwemo Clouds TV. Kama umefuatilia vipindi mbali mbali vya Clouds TV leo hii naamini umekwisha kutana na kuitazama video hiyo.Point ya msingi ni leo kwenye kipindi cha Clouds E ambapo Mwana FA alikuwepo ili kutusanua vitu ambavyo tulikuwa hatuvifahamu kuhusiana na video hiyo.
Unachotakiwa kukifahamu ni kwamba video hiyo imefanywa mara mbili na mmoja kati ya madirector wakubwa sana nchini South Africa baada ya version ya kwanza kutowaridhisha wakali hao.Mwana FA amedai kuwa video ambayo aliletewa mara ya kwanza hakuikubali kutokana na video hiyo kutoendana hata kidogo na idea ya wimbo na hivyo kulazimika kumwambia director huyo kuirudia tena video hiyo.
“Mara ya kwanza ilikuja lakini sisi hatukuwa tumeridhika na viwango ambavyo ilikuwa navyo kulinganisha na vile ambavyo sisi tulikuwa tunavihitaji. Sio viwango vya picha au nini lakini ni tafsiri ambayo sisi tulikuwa tunaipata kutoka kwenye wimbo haikkuwa tafsiri yenye kutosha kuwakilishwa na video ambayo tulikuwa nayo mara ya kwanza, kwahiyo ikabidi nisafiri tena kwaajili ya kushoot video nyingine.” Alisema Mwana FA.

SHARE


BOFYA LIKE KUUNGANA NASI FACEBOOK!


UNAIJUA BIASHARA YA FOREVER LIVING?....Kama una mtaji kuanzia 250,000 hadi 1,020,000 na unapenda kujikwamua na kubadilisha maisha yako kupitia biashara hii Tupigie simu nambari 0625539100 au 0625539200