MUONE HAPA RAIS MAGUFULI AKIMJULIA HALI LEO MKE WAKE MAMA JANETH MAGUFULI ALIYELAZWA MUHIMBILI | Masama Blog


MUONE HAPA RAIS MAGUFULI AKIMJULIA HALI LEO MKE WAKE MAMA JANETH MAGUFULI ALIYELAZWA MUHIMBILI


RAIS MAGUFULI AKIMJULIA HALI MKEWE MAMA JANNETH KATIKA HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI
Na Sosy
LIMEKUWA jambo la kawaida kwa viongozi mbalimbali na familia zao kutibiwa nje ya nchi au katika hospitali zinazotambulika kama za watu wenye hadhi na fedha lakini suala hili limekuwa tofauti kabisa kwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania John Magufuli.
Rais Magufuli amedhihirish uungwana uzalendo wake kwa kitendo cha mke wake kutibiwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Rais Magufuli ameonekana Hospitalini hapo leo akielekea wodini kujulia hali mkewe mama Janneth Magufuli.
suala hili limeonyesha kuwa Rais anawapenda wananchi wake kama anavyopenda nafsi yake ambapo mkewe amekuwa akipatiwa matibabu katika hospitali hiyo ambayo huwahudumia wananchi wote.
jambo ambalo limetofautiana viongozi wengi ambao hukimbilia kwenye hospitali za nje ya nchi
suala hili litazidi kuwapa imani wananchi kwa Rais wao kutokana na kuamini anachosimamia.Amepigania Hospitali ya Muhimbili kuwa hopitali itakayotoa huduma nzuri kwa wananchi wote.
Amepigania kuboresha mazingira ya matibabu katika hospitali hiyo. na hospitali nyengine nchini. 
Kama kawaida ya Rais Magufuli haikutosha kumona mkwe tu. aliwajulia hali na wagonjwa wengine.

BOFYA LIKE KUUNGANA NASI FACEBOOK!


UNAIJUA BIASHARA YA FOREVER LIVING?....Kama una mtaji kuanzia 250,000 hadi 1,020,000 na unapenda kujikwamua na kubadilisha maisha yako kupitia biashara hii Tupigie simu nambari 0625539100 au 0625539200