MTV KUMNYANG’ANYA TUZO WIZKID NA KUMPATIA ALI KIBA,ATANGAZWA NDIYE MSHINDI WA TUZO YA MTV EMA
Kituo cha runinga cha MTV kinatarajia kumpokonya mwanamuziki kutoka Nigeria, Wizkid tuzo aliyoshinda na kumkabidhi mwanamuziki Ali Kiba kutoka Tanzania baada ya kubainika kuwa mshindi halali wa tuzo hiyo ni Ali Kiba.Wizkid alitangazwa kushinda tuzo ya Mwanamuziki Bora wa Afrika iliyotolewa na MTV EMA (MTV Europe Music Awards) wakati wa utoaji tuzo uliofanyika mapema mwezi huu lakini kwenye tovuti ya MTV, mwanamuziki Ali Kiba ndiye alionekana mshindi.Baada ya hali hiyo kutokea watu wengi kupitia mitandao ya kijamii wameitaka MTV kutolea maelezo suala hilo kwani lilizua sintofahamu miongoni mwa mashabiki wa Ali Kiba.
Akizungumza leo usiku kupitia ukurasa wake wa Facebook, Ali Kiba alisema kuwa baada ya malalamiko mengi ya mashabiki, waandaaji wa tuzo za MTV EMA walimtumia ujumbe kuwa yeye ndiyo mshindi halali na kuwa tuzo hiyo italetwa nchini.Aidha, Ali Kiba amewashukuru mashabiki wake kwa kuwa naye bega kwa bega na kumpigia kura katika kila tuzo anazoshiriki.
Wanamuziki waliokuwa wakiwania tuzo hiyo ni Wizkid kutoka nchini Nigeria, Ali Kiba kutoka Tanzania, Back Cofee, Casper Nyovest wote kutoka Afrika Kusini na Olamide kutoka Nigeria.


Kujua Mbinu Za Kumfikisha Kileleni Mwanamke Kwa Haraka: BONYZA HPA CHNI

Kujua Sehemu 10 Zinazompa Raha mwanamke wakati wa Tendo, BONYZA HAP 1UU
BOFYA LIKE KUUNGANA NASI FACEBOOK!During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip.
© Copyright Masama Blog | Designed By MASAMA TEAM
Back To Top