Mtuhumiwa wa Madawa ya Kulevya apigwa risasi na kufa akijaribu kutoroka Mahakama ya Kisutu | Masama Blog


Mtuhumiwa wa Madawa ya Kulevya apigwa risasi na kufa akijaribu kutoroka Mahakama ya Kisutu

mtuhumiwa_madawa2mtuhumiwa_madawa1Machela_Kubeba_MaitiMtuhumiwa_Upande_mwingine
Mtuhumiwa wa Madawa ya kulevya amepigwa risasi na kufa papo hapo kufuatia kutaka kutoroka Mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam.
Tukio hili limetokea muda si mrefu.
Taarifa zaidi zinafuata…
=====
Mwendelezo:
Mdau Fikiri Liganga, anadai: "Inasikitisha sana. Nilikuwepo hapa Kisutu na kushuhudia huyo mtuhumiwa anatoroka hadi anauwawa”.
Anaendelea kuandika “Ilikuwa hivi: Huyo mshitakiwa ni raia wa Sierra Leone na aliletwa hapa Mahakamani kusomewa shitaka linalomkabili. Akaomba apelekwe msalani mara moja. Alipokuwa msalani akamsoma yule askari alokuwa anamsubiria nje na kuona kazubaa ndipo akaruka ukuta na kutoka nje na kuanza kukimbia. Mtuhumiwa alikuwa kavaa 'Jeans' akaivua kuona inamsumbua. Akakimbia akitaka kutokea katika lango kuu la Mahakama ya Kisutu lakini likafungwa haraka. Ndipo akaamua aende akaruke uzio wa pembeni ambao una vyuma vyenye ncha kali".
Fikiri anaongeza kuwa “Wakati huo wote askari walikuwa wanamfukuza kwa nguvu lakini hawakuweza kupiga risasi kwa sababu alikuwa mjanja sana akawa anakimbia katikati ya watu."
"Ndipo alipofika kwenye hyo fensi akijaribu kuruka askari akapiga risasi mbili hewani, jamaa hakutii. Ndipo akaiga risasi moja ikampata mkononi na nyingine mzima kampata tumboni na kufariki papo hapo."
Mdau Fikiri anasema kuwa msomaji ukitazama picha zinavyoonyesha, kakwama juu kwa sababu ile fensi ni ya chuma zenye ncha kali hivyo kuna chuma ilimchoma kwa ngyvu sana katika mguu hadi akawa ananing’inia vile."
mtuhumiwa_madawa2
Mtuhumiwa_Madawa_Kisutu
Mtuhumiwa_Akitolewa

BOFYA LIKE KUUNGANA NASI FACEBOOK!


UNAIJUA BIASHARA YA FOREVER LIVING?....Kama una mtaji kuanzia 250,000 hadi 1,020,000 na unapenda kujikwamua na kubadilisha maisha yako kupitia biashara hii Tupigie simu nambari 0625539100 au 0625539200