Mtoto wa Obama mwenye umri wa miaka 15 aamua kufanya kazi katika Mgahawa | Masama Blog

Mtoto wa Obama mwenye umri wa miaka 15 aamua kufanya kazi katika Mgahawa

Sasha Obama, mtoto wa Rais wa Marekani Barack Obama, ameamua kuacha ‘starehe’ za ikulu ya White House na kuanza kufanya kazi katika mgahawa mmoja, vyombo vya habari nchini Marekani vinaripoti.
Binti huyo mwenye umri wa miaka 15 ameanza kufanya kazi ya kuwahudumia wateja katika mgahawa mmoja ulioko Martha’s Vineyard, Massachusetts.
Sasha, ambaye anatumia jina lake kamili, Natasha, aliongozana na maafisa sita wa ulinzi wa secret service siku yake ya kwanza kazini, gazeti la Boston Herald linaripoti.
Picha zinazosambazwa zinamuonesha binti huyo  wa Obama akiwa amevalia sare ya hoteli akifanya kazi.
Mfanyakazi mmoja katika mgahawa huo aliambia gazeti hilo la Herald: “Tulikuwa tunashangaa ni kwa nini kulikuwa na watu sita walikuwa wanamsaidia msichana huyu, lakini baadaye tukagundua alikuwa nani.”
sashaaa

Back To Top