Mtoto mmoja amefariki huku mwengine akiuguza majeraha baada ya kudaiwa kupigwa na shangazi yao kwa kula mkate katika kijiji cha Kiganjo kaunti ya Murang’a nchini Kenya.
Kwa mujibu wa luninga ya NTV nchini Kenya,Mtoto huyo wa miaka mitatu alifariki kutokana na majeraha aliyopata kwenye kichwa huku kaka yake mwenye umri wa miaka 5 akiwa amelazwa katika hospitali ya Nyeri.
Wawili hao wanadaiwa kupigwa na shangazi huyo ambaye amedaiwa kuwa na matatizo ya akili.
Majirani wanasema kuwa waliwasikia wavulana hao wakipiga kelele na kwenda kuwaokoa na kuwakuta  wamelala ardhini wakiwa hawana fahamu.
Runinga hiyo inasema kuwa kulingana na mkazi mmoja wa eneo hilo watoto hao walikuwa wameachwa nyumbani na bibi yao ili kukaa na shangazi yao.
Nilikuwa nimeenda kununua dawa ya mtoto mmoja kati yao baada ya ngozi yake kukumbwa na upele kabla ya kupata simu kutoka kwa mmoja wa jirani zangu akinielezea kilichotokea,alisema bibi
Kwa mujibu wa wakazi wa eneo hilo wanadai Shangazi huyo aliwapiga wavulana hao baada ya kula mkate ambao ulikuwa wake.

BOFYA LIKE KUUNGANA NASI FACEBOOK!


Je wewe una mtaji wa Ths.250,000/= au 510,000 au 1,020,000?..na unahitaji kufanya biashara kubwa kwa mtaji huo ufanikiwe?..basi kama ndiyo njoo tukuonyesha njia ya kutekeleza malengo yako...piga 0625 539 100

 
Top