Kuna mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 10 ametinga hadi Idara ya Hekaheka nakutaka msaada wa kumpata baba yake ambaye ni msanii mkubwa wa bongo Movie.
Mtoto anadai aliambiwa na rafiki wa mamayake kuwa  baba yake ni Cheki Budi.Mpaka ameamua kuja kutaka msaada ni kwa kuwa mamayake hajawahi kumwambia chochote kuhusu babayake na hata akimuuliza huwa anamzuga tu.
Idara ya Hekaheka ilifunga safari na mtoto huyo hadi nyumbani kwao na kuonana na mamayake ili kutaka kujua stori kamili
Mama wa mtoto huyo alishtuka na kitendo cha mwanae kwenda kumtafuta babayake kwakuwa yeye mwenyewe hakuwahi kumwambia chochote japo alikuwa akimsumbua kila siku lakini hakuwahi kumtajia na wala hakupenda mtoto wake aje aambiwe kutokana na mazingira ya yeye alipokutana na Cheki budi kipindi hicho.
Mama anasema ilikuwa mwaka 2005 ndipo alikuja Dar kwa mara ya kwanza akitokea Singida ambapo alikuwa ameshaolewa.Siku moja alienda kwa rafiki yake kumtembelea ilipofika usiku shosti alimpeleka Club na huko ndipo shogayake  huyo alimuunganishia na Cheki budi na siku hiyohiyo alipata ujauzito.Na kesho kutwa yake alirudi zake Singida kwa mume wake.
Alijifungua mtoto wake na baada ya kufikisha miezi 6 wifi zake waligundua kuwa mtoto sio wa kakayao kwahiyo kiliitishwa kikao ikabidi apewe talaka.Ikambidi aanze maisha ya mapya huku akimlea mtoto wake mwenyewe hadi alipofikisha miaka miwili ndipo alipata mume mwingine ambaye ndio yupo nae hadi sasa
Mama anasema mtoto amekuwa akimsumbua siku nyingi kutaka kumjua babayake lakini hajawahi kumwambia na wala alikuwa hataki kabisa mtoto wake aambiwe kitu chochote kwakuwa alikutana na Chekibudi kwa bahati mbaya tu na hata yeye mwenyewe kipindi hicho alikuwa hamjui kuwa ni nani.
Rafiki yake huyo ambaye ndiye aliyemuunganisha kipindi hicho ndiyo huyohuyo aliyemtonya mtoto kuwa babayake ni Checkbudy.Mama anasema alishaagombana nae kutokana na tabia zake za kumlazimisha kuwa amwambie mtoto ukweli.
photogrid_14791147883541
Huyu ndiye mtoto mwenyewe ambaye inadaiwa babayake ni Msanii  Cheki Budi
Sikiliza hapa kisa kizima
Mamawa mtoto
Audio Player
00:00
00:00
Use Up/Down Arrow keys to increase or decrease volume.
Audio Player
00:00
00:00
Use Up/Down Arrow keys to increase or decrease volume.
Audio Player
00:00
00:00
Use Up/Down Arrow keys to increase or decrease volume.
Audio Player
00:00
00:00
Use Up/Down Arrow keys to increase or decrease volume.
Audio Player
00:00
00:00
Use Up/Down Arrow keys to increase or decrease volume.
Mtoto >>Zena (rafiki wa mama) ndio aliniambia kuwa unamjua baba yako?Nikamwambia mi simjui akaniambia usimwambie mamayako hii ni siri nakwambia baba yako ni Chekibudi,basi mimi nikarudi nyumbani….
Nilimuuliza mama Nielekeze Clouds ipo wapi siku moja nataka kwenda kwenye michezo nikatolewa ndio akanielekeza…
Mimi nataka tu nimuone tu basi huyo Chekibudi (babaangu) na nikimuona tu nitamuuliza unanijua mimi akisema hanijui ntamuuliza unamjua mamaangu,akikataa basi akikubali ntafrahi…
Audio Player

BOFYA LIKE KUUNGANA NASI FACEBOOK!


Je wewe una mtaji wa Ths.250,000/= au 510,000 au 1,020,000?..na unahitaji kufanya biashara kubwa kwa mtaji huo ufanikiwe?..basi kama ndiyo njoo tukuonyesha njia ya kutekeleza malengo yako...piga 0625 539 100

 
Top