MTOTO DREAM WA BLAC CHYNA AWAVURUGA AMBER ROSE NA KHLOE KARDASHIAN | Masama Blog


MTOTO DREAM WA BLAC CHYNA AWAVURUGA AMBER ROSE NA KHLOE KARDASHIAN


Kitendawili cha Amber Rose au Khloe Kardashian nani atakua Mama Wa Ubatizo Wa Mtoto Dream wa Blac Chyna na Rob Kardashian bado ni tatizo.
Inaonesha kama Rob na Chyna wanaweza kuingia kwenye mgogoro mwingine siku za hivi karibuni.
“Rob na Blac Chyna ndio wenye maamuzi ya kumchagua nani awe mama wa ubatizo wa mtoto wao kati ya Amber Na Khloe”Wote wanajua ni kiasi gani Khloe anaitaka nafasi hiyo sio tu kwasababu ni dada wa Rob, Amekua ni zaidi ya mshikaji wa muda mrefu na Rob, lakini upande wa pili unadai Amber Rose nae ni zaidi ya dada kwa Blac Chyna,
Japo hakuruhusiwa kwenda kumuona mtoto mara tu alipozaliwa,Lakini Amber Rose alipata fursa ya kumuona Mtoto kwa muda wake na kupoa nae kwenye picha tofauti tofauti ” Chanzo cha karibu na familia hiyo kimeuambia mtandao wa boosip.

Amber na Khloe wamekuwa na beef kwenye mitandao ambayo imehusisha mpaka ishu za familia kama unavyoweza kwenye baadhi ya hizi tweets hapa chini.Ambe Rose amewahi kuwa girlfriend wa Rapa Kanye West ambae sasa ni mume wa Kim Kardashian dada wa Khloe..
hata hivyo wachambuzi wa masuala ya kifamilia wanadai huenda mtoto Dream akawa chanzo chanzo cha kumaliza kabisa tofauti zaoo au kutengeneza beef ya waziwazi iwapo maamuzi ya kuchagua mama wa ubatizo yataelemea upande mmoja.

BOFYA LIKE KUUNGANA NASI FACEBOOK!


UNAIJUA BIASHARA YA FOREVER LIVING?....Kama una mtaji kuanzia 250,000 hadi 1,020,000 na unapenda kujikwamua na kubadilisha maisha yako kupitia biashara hii Tupigie simu nambari 0625539100 au 0625539200