MSIKIE HAPA MR NICE AKIFUNGUKA KUHUSU ZIARA YA RAIS MAGUFULI KENYAMsanii mkongwe wa muziki nchini, Mr Nice ambaye kwa sasa anafanya muziki wake nchini Kenya, amefunguka na kuzungumzia shamra shamra za mapokezi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli ambaye yupo nchini nchini Kenya kwa ajili ya ziara ya kikazi.
Rais Magufuli amekuwa akijizolea umaarufu katika nchi mbalimbali za Afrika kutokana na utendaji wake wa kazi pamoja na jitihada za kupambana na janga la rushwa.
Akizungumza na Bongo5 Jumanne hii, Mr Nice amesema Wakenya wamempokea Rais Magufuli kwa shangwe kutokana na Wakenya wengi kuukubali utendaji wake wa kazi.
“Magufuli tumempokea kwa shangwe nyingi sana na Wakenya wamemfagilia ile mbaya kabisa, kila mtu amekuwa akisubiria ujio wake so jana alipoingia nilipigiwa simu nyingi sana na ujumbe kibao kila mtu akiniambia baba yako magufuli amekuja kujua maendeleo yako huku,” alisema Mr Nice.
Aliongeza, “Yaani nimefarijika sana. Huku jina limekuwa sasa ni Mr Nice wa Magufuli wala si Mr Nice wa TZ tena kama walivyozoea kuniita,”
Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri nchini Kenya, ameendelea kufanya show mbalimbali nchini humo ambapo wiki hii anatarajia kuwa na show kubwa maeneo ya Kisii pamoja na Nakuru.


Kujua Mbinu Za Kumfikisha Kileleni Mwanamke Kwa Haraka: BONYZA HPA CHNI

Kujua Sehemu 10 Zinazompa Raha mwanamke wakati wa Tendo, BONYZA HAP 1UU
BOFYA LIKE KUUNGANA NASI FACEBOOK!During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip.
© Copyright Masama Blog | Designed By MASAMA TEAM
Back To Top