sadifa-6
NA IMELDA MTEMA | RISASI JUMAMOSI: WIKI hii tumefunga safari mpaka visiwani Zanzibar, ambapo imeenda kuyadadavua maisha halisi ya mbunge wa Donge na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Taifa (UVCCM), Sadifa Juma.

Mbunge huyo mwenye umri wa miaka 35, anaishi Uwanja wa Ndege visiwani humo akiwa na mkewe kipenzi aitwaye Salma pamoja na watoto wake wawili ambao ni  mapacha waitwao Sammy na Sameer (2). Bila hiyana mbunge huyo alianza kuelezea maisha yake ya kila siku nje ya siasa. Ungana nami hapa chini kwa kujua mengi zaidi:

 Anapata muda wa kukaa na familia yake kutokana na kazi yake ya siasa?

“Kiukweli kabisa muda wa kukaa na familia yangu ni mdogo sana mara nyingi nakuwa kwenye kazi na kama kukaa nayo ni muda mchache sana lakini kwa sababu ni kazi inabidi iwe hivyo maana sina namna nyingine.

Mke hapati shida kutokana na muda wake mdogo kwa familia?

“Mke wangu niko naye sasa miaka minne  lazima tu atakuwa amezoea na anajua taratibu zangu, hana shida japokuwa najua kabisa kuna wakati anapokosa uwepo wangu ananimisi na hata mimi kuna kipindi naikumbuka sana familia yangu.

 Akiwa na Wananchi jimboni kwake.

Nini anachopenda anapokuwa nyumbani kwake?

“Kutokana na kutokuwa muda mwingi na familia yangu ninapokuwa nyumbani muda mwingi natumia kucheza na wanangu na kukaa na mke wangu kujadili vitu mbalimbali vya maisha yetu.

 Ni chakula gani anapendelea kula anapokuwa nyumbani kwake?

“Mimi jiko la jeshi bwana sichagui chakula, chochote nakula mradi tu kisiwe na sumu lakini sina tabia ya kutaka hiki na hiki sikitaki, vyote nakula.
 Anazungumziaje wanaosema yeye ni mlevi?

“Ndio mimi ni mlevi wa mafanikio ya jimbo langu na si vinginevyo.
 Anamsaidia mkewe kupika, kufua?

“Dooh sitaki kudanganya kabisa mimi sijawahi kuingia kupika au kufua kwa sababu hata mke wangu mwenyewe hafanyi hivyo vitu, wapo watu wanaomsaidia lakini kama siku nitakuwa peke yangu kabisa hakuna mtu, naweza kufanya hivyo vitu.

akikagua-mradi-wa-umeme-jimboni-kwakeVipi kuhusu kudaiwa ni mkali kupitiliza?

“Hapana ukali wa nini sasa jamani ndio maana nasema kuwa mtu anaweza kutafsiri tofauti mimi sina ukali wowote zaidi zaidi muda wote ni kufurahi na watoto wangu na ndio maana unaona kutwa hawawezi kubanduka wakiniona sehemu.

 Akioa wake wawili ataweza kugawa upendo wake?

“Unajua ni hivi hata kabla ya kuoa unashauriwa kuwa kama huwezi kuhudumia mke utakayemuongeza ni bora uwe na mmoja hivyo unapoamua kuoa mke mwingine ni lazima chochote anachopata mwenzake naye apate na upendo uwe hivyohivyo hivyo ikitokea nimeoa wa pili lazima nitaweza kumhudumia.

 Anapendelea mavazi gani zaidi nyumbani?

“Kama unavyoniona hapa mimi bado ni kijana kabisa napendelea zaidi mavazi ya vijana kama tisheti na jinzi naona nikivaa ndio vinanitoa zaidi.

Nini anachokitamani katika maisha yake ya kila siku?    

“Natamani sana amani ndani ya familia yangu na pia natamani pia kila kitu ambacho niliwahaidi wananchi wa jimbo langu nikitimize kwa wakati kwa maana hata muda wangu ukiisha nijue kuna kitu nilikifanya katika jimbo langu.”
BOFYA LIKE KUUNGANA NASI FACEBOOK!


Je wewe una mtaji wa Ths.250,000/= au 510,000 au 1,020,000?..na unahitaji kufanya biashara kubwa kwa mtaji huo ufanikiwe?..basi kama ndiyo njoo tukuonyesha njia ya kutekeleza malengo yako...piga 0625 539 100

 
Top