Mshtakiwa shauri la mauaji ya Dk Mvungi aomba kurejea mtaani | Masama Blog


Mshtakiwa shauri la mauaji ya Dk Mvungi aomba kurejea mtaani


Aliyekuwa mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, marehemu Dk Sengondo Mvungi. 

Dar es Salaam. Mmoja wa washtakiwa 10 wanaokabiliwa na kesi ya mauaji ya kukusudia ya aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Dk Sengondo Mvungi ameiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwaachia ili warejee mtaani.

Masunga Makenza (40), alitoa ombi hilo jana mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba baada ya Wakili wa Serikali, Patrick Mwita kuieleza Mahakama kuwa jalada la kesi yao awali lilikuwa kwa Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mkoa (RCO) na sasa lipo kwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) kusubiri uamuzi.

Baada ya kutolewa maelezo hayo, Makenza alisema: “Tunaomba leo hii tuachiwe,  twende mtaani kufuatia kauli ya Rais ya Hapa Kazi Tu, kwa kasi hii ya upande wa mashtaka hatutafika.  Tunaomba tuondoke wakikamilisha upelelezi watatukamata tena mtaani.”

BOFYA LIKE KUUNGANA NASI FACEBOOK!


UNAIJUA BIASHARA YA FOREVER LIVING?....Kama una mtaji kuanzia 250,000 hadi 1,020,000 na unapenda kujikwamua na kubadilisha maisha yako kupitia biashara hii Tupigie simu nambari 0625539100 au 0625539200