Mshindi wa Tuzo ya Nobel Profesa Wole Soyinka Adai 'Nitaondoka Marekani Trump akiapishwa' | Masama Blog


Mshindi wa Tuzo ya Nobel Profesa Wole Soyinka Adai 'Nitaondoka Marekani Trump akiapishwa'


Mshindi wa Tuzo la Nobel na mwandishi raia wa Nigeria Wole Soyinka, anasema kuwa ataondoka Marekani siku ambayo Donald Trump ataapishwa kuwa rais.

Wiki iliyopita Soyinka aliahidi kuwa angeirarua green Card yake, ikiwa Trump angechaguliwa kuwa rais wa Marekani.

Green Card humpa mtu kibali ya kuishi rasmi nchini Marekani na hupewa umuhimu mkubwa na wahamiaji kutoka nchi za Afrika.

Soyinka alitoa matamshi hayo wakati akihutubia wanafunzi katika chuo cha Oxford nchini Uingereza.

Mwandishi huyo maarufu alionekana kuchukua msimamo mkali kupinga seza za uhamiaji za bwana Trump.

Soyinka alishinda tuzo la Nobel la fasihi mwaka 1986 na kuwa mwafrika wa kwanza kupata tuzo hilo.

BOFYA LIKE KUUNGANA NASI FACEBOOK!


UNAIJUA BIASHARA YA FOREVER LIVING?....Kama una mtaji kuanzia 250,000 hadi 1,020,000 na unapenda kujikwamua na kubadilisha maisha yako kupitia biashara hii Tupigie simu nambari 0625539100 au 0625539200