MSANII Q-CHILLA ASEMA HAJAWAHI KUOMBA KOLABO KWA WABONGO | Masama Blog


MSANII Q-CHILLA ASEMA HAJAWAHI KUOMBA KOLABO KWA WABONGO


Msanii nguli wa bongo fleva Q Chilla amesema hajawahi kumpigia msanii yoyote hapa Tanzania kumuomba wafanye kolabo japo yeye amekuwa akipokea simu nyingi kutoka kwa wasanii mbalimbali wakimuomba kufanya naye kolabo.

Q Chilla
Akiongea ndani ya eNewz Q Chilla amesema huwa ana angalia muda wake pale anapo pigiwa simu za kuombwa kolabo na mara nyingi ana angalia malipo na muda.
Q Chilla pia alisema aliamua kuchukua maoni ya watu walipo mshauri kuwa akitaka kupiga kolabo afanye na Diamond kwa kipindi hiki, ndiyo akaamua kuufanyia kazi ushauri wa mashabiki zake.
Mbali na hayo pia Q Chilla hakusita kumsifia King Kiba kuwa ana stahili kuwa KING na anapenda ngoma zake ila kuna utofauti kati yao hivyo watakapo kutana kwenye kolabo ni lazima wafanye wimbo wa tofauti sana kwa kuwa wote ni wakali wa voko.

BOFYA LIKE KUUNGANA NASI FACEBOOK!


UNAIJUA BIASHARA YA FOREVER LIVING?....Kama una mtaji kuanzia 250,000 hadi 1,020,000 na unapenda kujikwamua na kubadilisha maisha yako kupitia biashara hii Tupigie simu nambari 0625539100 au 0625539200