MSANII MAUA SAMA AFUNGUKA HAYA KUHUSU RUBY | Masama Blog


MSANII MAUA SAMA AFUNGUKA HAYA KUHUSU RUBY

14730740_738420099643409_1139081384812347392_n
Maua Sama amedai kuwa licha ya kuondoka kwa Ruby THT, kundi lao la Butterfly halijafa.

Maua ametoa taarifa hizo kupitia kipindi cha Vibe la Kitaa cha ABM Radio ya Dodoma kinachoendeshwa na Dj Rodger. Amedai kuwa kwa sasa kila member anafanya kazi zake za solo na amesema hivi karibuni kulikuwa na mambo mengi ikiwemo Fiesta.
“Project bado ipo hai na inaendelea na wakati wa msimu wa Fiesta tulikuwa tunaendelea kuipa promo kama kawaida na kulikuwa kuna project ya Kipepeo ambayo tulikuwa tunatembea kila shule katika mikoa tuliyopita kwenye Fiesta kwaajili ya kuwahiza wanafunzi ,” amesema Maua.
“Kwahiyo haimaanishi kuwa sababu Ruby ameondoka THT basi na project ya Butterfly imekufa, hiyo sio kweli,” amesisitiza.
Kundi hilo sasa limebakiwa na Maua, Nandy na Alice.

BOFYA LIKE KUUNGANA NASI FACEBOOK!


UNAIJUA BIASHARA YA FOREVER LIVING?....Kama una mtaji kuanzia 250,000 hadi 1,020,000 na unapenda kujikwamua na kubadilisha maisha yako kupitia biashara hii Tupigie simu nambari 0625539100 au 0625539200