Msanii mkongwe kutoka Uganda Dk.Jose Chameleone, mbali ya kuwa na utajiri wakupindukia, lakini bado amedhihirisha kuwa ndoto yake haijatimia ya kuongeza ukwasi wake.

Jana kupitia mtandao maarufu wa kijamii wa Instagram alidokeza kidogo kupitia ukurasa wake kwa kuweka kipande cha video kilichoonesha bidhaa hiyo huku akiandika XOS Chameleone 2017 #SmartPhone Yuh ready???.
Jose Chameleone
Hata hivyo mkali huyo wa Valu Valu bado hajaweka wazi specifications ya simu hiyo, Hivyo nakusihi uwe sanjari nasi kukujuza vingi kuhusiana na bidhaa hiyo.
Mbali na Chameleone pia Mkali wa wimbo Salome, Diamond Platnumz siku kadha hapo nyuma aliweza kuonyesha sample yake ya kwanza ya bidhaa yake mpya ya perfume ‘ChibuPerfume’ inayotarajiwa kuingia sokoni siku za usoni.
Muimbaji huyo aliwataka mashabiki wa muziki wake kukaa tayari kwa ajili ya ujio wa bidhaa hiyo ambayo itapatikana katika maduka mbalimbali ya vipodozi nchini.
Kumbuka Jose Chameleone ndiye msanii tajiri zaidi kuliko msanii yeyote hapa Afrika Mashariki hivyo tutarajie mapinduzi kutoka kwake kwani ni hatua nzuri kwa wasanii wetu.
15046832_1344674128916422_7192795358542430208_n

Mbali na hilo pia Jose Chameleone anatarajia kuachia ngoma yake mpya aliyoipa jina la ‘Sweet Banana’ mwakani 2017

BOFYA LIKE KUUNGANA NASI FACEBOOK!


Je wewe una mtaji wa Ths.250,000/= au 510,000 au 1,020,000?..na unahitaji kufanya biashara kubwa kwa mtaji huo ufanikiwe?..basi kama ndiyo njoo tukuonyesha njia ya kutekeleza malengo yako...piga 0625 539 100

 
Top