MSANII GABO KUZIBA BENGO LA MAREHEMU STEVEN KANUMBA | Masama Blog


MSANII GABO KUZIBA BENGO LA MAREHEMU STEVEN KANUMBA

14291912_663339300495519_6955797915967746303_n
Msanii wa filamu anayefanya vizuri na filamu ‘Safari ya Gwalu’ Salim Ahmed aka Gabo Zigamba amefunguka kwa kusema kuwa wasanii wa filamu wakiwa na juhudi wanaweza kuziba pengo la marehemu Steven Kanumba.
Mwigizaji huyo ambaye ni miongoni mwa wasanii wa filamu ambao wanafanya vizuri kwa sasa, amedai kama wasanii wakiamua kufanya kazi kwa bidii basi kila kitu kinawezekana.
“Pengo la marehemu Kanumba litazibika tu ingawa najua tobo la panya huwezi kuziba na mkate ila tutajitahidi kuziba,” Gabo alimjibu shabiki katika Kikaango cha EATV.
Aliongea,”Niwashauri watu wawe makini kwenye nidhamu, wawe makini kwenye elimu na pia wasikate tamaa katika mambo wanayofanya”
Mwigizaji huyo amemtaja Single Mtambalike kuwa ndiye mwigizaji wake bora kwa sasa

BOFYA LIKE KUUNGANA NASI FACEBOOK!


UNAIJUA BIASHARA YA FOREVER LIVING?....Kama una mtaji kuanzia 250,000 hadi 1,020,000 na unapenda kujikwamua na kubadilisha maisha yako kupitia biashara hii Tupigie simu nambari 0625539100 au 0625539200