MSANII DOGO JANJA ATAMANI NDOA AKIWA NA UMRI MDOGO | Masama Blog


MSANII DOGO JANJA ATAMANI NDOA AKIWA NA UMRI MDOGO

dogo-janjaMsanii wa muziki wa kurap kutoka Tip Top Connection, Dogo Janja amesema ni lazima aingie kwenye maisha ya ndoa akiwa na umri mdogo.Rapa huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo Kidebe, amesema kwa sasa hana muda mrefu ataingia kwenye maisha ya ndoa kwani tayari ameshajianda kukabiliana na changamoto za ndoa.“Hakuna haja yakuogopa, mimi lazima nioe nikiwa na umri mdogo ndo nimepanga hivyo,” alisema. “Kwanza ni jambo ambalo linampendeza mwenyezi Mungu kwa hiyo ukifika wakati wakufunga ndoa nitafanya hivyo,”Aliongeza, “Mimi naamini maisha ni haya haya, tena usishangae ukioa mambo yakakunyokea zaidi, kwa hiyo mimi nimesema muda ukifika nafunga ndoa,”Rapa huyo amesema Tunda Man aliyefunga ndoa hivi karibuni amemfanya nayeye afikirie kuoa siku za usoni.

BOFYA LIKE KUUNGANA NASI FACEBOOK!


UNAIJUA BIASHARA YA FOREVER LIVING?....Kama una mtaji kuanzia 250,000 hadi 1,020,000 na unapenda kujikwamua na kubadilisha maisha yako kupitia biashara hii Tupigie simu nambari 0625539100 au 0625539200