Mkuu Wa wilaya ya Kigamboni Mhe Hashim Mgandilwa, leo tarehe 8/11/2016 amefanya ziara katika Kata ya Kibada ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya kutembelea Kata mbalimbali za Wilaya ya Kigamboni ili kushirikiana na wananchi katika shughuli za kimaendeleo, kusikiliza na kutatua kero zao moja kwa moja kwa kuwafuata wananchi walipo.

DC Mgandilwa ameshiriki katika ujenzi wa vyumba 3 vya madarasa kwenye shule ya Msingi Mizimbini ambapo ameshirikiana na wananchi kusomba matofali, maji na kisha ujenzi wa kuta kwa kushirikiana na mafundi.  Vyumba hivyo vya madarasa vinajengwa kwa nguvu za wananchi na viko katika hatua za mwisho kukamilika.

DC Mgandilwa pia amezindua chumba kimoja cha darasa ambacho kimejengwa kwa fedha iliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe John Pombe Magufuli.

DC alikataa kukubaliana na taarifa ya ujenzi wa chumba hicho cha darasa iliyotaja kuwa pesa yote iliyotolewa kwa ajili ya ujenzi illitumika ikaisha kabla ya ujenzi kukamilika kisha wakaomba pesa nyingine kwa diwani iliyosaidia kukamilisha ujenzi huo. 

"......pesa iliyotolewa ilikuwa imepigiwa mahesabu ya kuanza msingi Mpaka ujenzi kukamilika, iweje hapa haikutosha na katika maeneo mengine ilitosha?.....hii haiwezekani na lazima waliohusika na hujuma hizi wawajibike.... " Alisisitiza Mgandilwa

DC Mgandilwa ameagiza wakaguzi wa mahesabu kutoka halmashauri ya manispaa ya Kigamboni kwenda shuleni hapo na kuhakiki gharama zilizotumika kama ni kweli ili kama kuna ubadhilifu wowote hatua kali za kisheria zichukuliwe dhidi ya wahusika.

Katika Mkutano wa hadhara, DC Mgandilwa amewataka wananchi kuendelea kujitoa katika shughuli za kimaendeleo pale wanapoombwa na viongozi wao kufanya hivyo
Amesema yeye na uongozi mzima wa wilaya ya Kigamboni wako tiyari kushirikiana na wananchi katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo na pale watakaokuwa na shughuli kama hizo wasisite kuwaalika ili washirikiane nao.

Ziara ya Mkuu wa wilaya inalenga kumpa fursa DC kushirikiana na wananchi katika shughuli za kimaendeleo, kusikiliza na kutatua kero zao moja kwa moja katika maeneo wanayoishi.

BOFYA LIKE KUUNGANA NASI FACEBOOK!


Je wewe una mtaji wa Ths.250,000/= au 510,000 au 1,020,000?..na unahitaji kufanya biashara kubwa kwa mtaji huo ufanikiwe?..basi kama ndiyo njoo tukuonyesha njia ya kutekeleza malengo yako...piga 0625 539 100

 
Top