MBUNGE LEMA ANUSURIKA KUTEKWA, AOKOLEWA NA POLISIMbunge wa Jimbo la Arusha Godbless Lema usiku wa kuamkia leo, amenusurika kutekwa na Majambazi eneo Makuyuni Wilayani Monduli akitokea Bungeni Dodoma.
Akisimulia tukio hilo, amesema alitoka Dodoma saa moja usiku na kufika Makuyuni saa saba usiku wa kuamkia leo, ndipo mita hamsini kutoka kizuizi cha Polisi, alikuta mawe makubwa barabarani na malori mawili yamesimama, akagundua ni majambazi na kuamuru dereva kugeuza gari lake.
Amesema alikuwa katika gari namba T.114 DGR Land Cruser V8, ambalo waliona watu zaidi ya kumi wakitoka pembeni ya barabara wakiwa na marungu na mapanga wakiturushia mawe, lakini tulifanikiwa kukimbia na kutoa taarifa Polisi, ambao walifanikiwa kumuua Jambazi mmoja.
Kamanda wa Polisi, Charles Mkumbo amekiri kutokea kwa tukio hilo na kudai wamepata taarifa kwa raia wema ambapo Polisi wa doria waliwahi kufika eneo la tukio na kufanikiwa kumuua jambazi mmoja ambaye jina lake halijafahamika mara moja katika majibizano ya risasi na Polisi.

Amesema jambazi huyo akiwa na wenzake 29 wakiwa na bunduki ambayo aina yake haijajulikana na silaha za jadi,, huku wakiwa wameweka mawe barabarani, walisimamisha gari aina ya fuso lenye namba T.871 BUZ lililokuwa likitoka Moshi kwenda Singida likiwa na mzigo mzito na kumpora abiria mmoja Victor Pius (46) Mfanyabiashara, Mkazi wa Majengo Mosho.

Pia abiria huyo aliporwa simu mbili aina ya Nokia na Samsung na fedha tasilimu shlingi 50,000.

Amesema pia wamefanikiwa katika tukio hilo kukamata majambazi 12 papo hapo wakiwa na mapanga sita na marungu manne.


Kujua Mbinu Za Kumfikisha Kileleni Mwanamke Kwa Haraka: BONYZA HPA CHNI

Kujua Sehemu 10 Zinazompa Raha mwanamke wakati wa Tendo, BONYZA HAP 1UU
BOFYA LIKE KUUNGANA NASI FACEBOOK!During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip.
© Copyright Masama Blog | Designed By MASAMA TEAM
Back To Top