Wanasayansi nchini India wamegundua kwamba chembe za protini za maziwa kwenye mende zina virutubisho vingi sana ambavyo vinaweza kutumiwa kama tembe ama chakula chenye virutubisho vya protini kwa kiwango cha juu.

Wanasayansi katika taasisi ya sayansi ya seli katika mji wa Bengaluru, wamefanya ugunduzi huo baada ya kutafiti muundo wa chembe za protini zinazopatikana katika utumbo wa aina ya mende wajulikanao kama Diploptera puncata, ambao ndio pekee hujifungua.

Ingawa mende kwa kawaida hawatoi maziwa, mende aina ya Diploptera puncata huwa wanatengeneza aina fulani ya maziwa yenye protini kwenye utumbo, ambayo hutumiwa kulisha watoto wake.

Chembe moja ya protini hiyo inakadiriwa kuwa na kiwango mara tatu cha nguvu ya mwili ikilinganishwa na kiasi sawa cha maziwa ya nyati.Chembe hizo zina nguvu mara nne kushinda maziwa ya ng’ombe.Matokeo ya utafiti huo yamechapishwa katika jarida la kimatibabu la International Union of Crystallography.
BOFYA LIKE KUUNGANA NASI FACEBOOK!


Je wewe una mtaji wa Ths.250,000/= au 510,000 au 1,020,000?..na unahitaji kufanya biashara kubwa kwa mtaji huo ufanikiwe?..basi kama ndiyo njoo tukuonyesha njia ya kutekeleza malengo yako...piga 0625 539 100 
Top