Matokeo ya awali yameendelea kutolewa katika Uchaguzi Mkuu wa Marekani uliofanyika jana, ambapo hadi asubuhi hii mgombea urais wa Republican, Donald Trump alikuwa akiongoza kwa majimbo 60 dhidi 48 ya Hillary Clinton wa Democratic.
Mbali na kuongoza katika majimbo hayo, wakati asilimia 89 ya kura zilikuwa zimehesabiwa mgombea huyo alikuwa akiongoza katika Jimbo la Florida kwa kura 18,000 zaidi dhidi ya Hillary; jimbo ambalo ili mgombea ashinde urais wa Marekani ni lazima apate ushindi jimboni humo.
Kambi ya Trump pia ilikuwa ikidai kuwa angeshinda katika majimbo ya Alabama, Arkansas, Indiana, Kentucky, Mississippi, Missouri, Oklahoma, South Carolina, Tennessee and West Virginia.
Matokeo yaliyokuwa bado kuthibitishwa katika majimbo ya Delaware, Rhode Island, Illinois, Maryland, Massachusetts, New Jersey, Rhode Island, Vermont na District of Columbia yalionyesha kumpa ushindi Hillary.
Ili mshindi apate ushindi atatakiwa kupata ushindi unaofahamika kama ‘electoral college’ wa 270 dhidi ya mpinzani wake

BOFYA LIKE KUUNGANA NASI FACEBOOK!


Je wewe una mtaji wa Ths.250,000/= au 510,000 au 1,020,000?..na unahitaji kufanya biashara kubwa kwa mtaji huo ufanikiwe?..basi kama ndiyo njoo tukuonyesha njia ya kutekeleza malengo yako...piga 0625 539 100

 
Top