Ticker

10/recent/ticker-posts

Maambukizi ya virusi vya UKIMWI yashamiri Simiyu, chanzo chatajwa

Mkoa wa Simiyu ni miongoni mwa mikoa yenye ushamiri wa maambukizi ya virusi vya ukimwi yanayosababishwa na tabia ya wanaume wenye umri kati ya miaka 15 hadi 49 walio wengi kutokuwa na utamaduni wa kufanyiwa tohara ,hivyo kuwa chanzo kikuu cha kuenea kwa maambukizi ya vvu na ukimwi ,ambapo tohara hukinga kwa asilimia 60.


Akizungumza kwenye uzinduzi wa mkutano wa wadau wa mapambano dhidi ya ukimwi na uzinduzi wa mpango mkakati wa mkoa ,mkuu wa mkoa wa simiyu Anthony mtaka amesisitiza jamii kuwahamasisha wanaume ambao hawajapata tohara kwenda kufanyiwa ili kuondoa hatari ya maambukizi kiurahisi .

screen-shot-2016-11-24-at-1-53-34-pm

Aidha mtaka amewataka wadau na wazazi kuwapa ujasiri watoto wanapoamua kuwa na mahusiano kwa kuwaeleza bayana kuhusu matumizi sahihi ya kondomu na wanapofikia maamuzi ya kuoana ni vema wapime ili kujua afya zao ,hali ambayo italiepusha taifa na vifo vinatokanavyo na vvu na inapobainika mmojawapo ana maambukizi itasaidia kuanza dozi mapema.

Akiongea kwa niaba ya mganga mkuu wa mkoa wa Simiyu, mratibu wa kudhibiti ukimwi wilaya ya bariadi Wilfred Magulu amesema katika kiwango cha tohara kwa mawanaume kisayansi mwanaume anapotahiriwa kuna uwezekano mkubwa wa kutopata maambukizi kwa asilimia 60 ,hivyo lipo zoezi endelevu katika vituo mbali mbali vya afya na zahanati.

Kushamiri kwa maambukizi ya vvu kimkoa ni asilimia 3.6 ambapo wilaya ya busega ina asilimia 5.8 na hivyo kuzidi ushamiri kitaifa ambaao ni asilimia 5.1.