London derby- Je, Spurs kufuta rekodi mbaya dhidi ya Chelsea Darajani?Ligi Kuu ya England leo inaendelea kwa michezo sita kuchezwa katika viwanja tofauti. Ndani ya michezo hiyo kuna pambano la mahasimu wa jadi wa jiji la London Chelsea dhidi ya Tottenham Hotspur litakalofanyika katika Uwanja wa Stamford Bridge majira ya saa 2.30 za usiku.

Kuelekea pambano hilo kuna takwimu muhimu ambazo kila timu inajivunia kutoka kwa hasimu wake.

Dondoo muhimu za kufahamu
Tottenham hawajashinda Stamford Bridge tangu February 1990.
Chelsea hawajafungwa na Spurs kwenye michezo 26 ya nyumbani (wameshinda 17, droo 9). Hii ni rekodi kubwa zaidi kuliko timu yeyote.
Chelsea

Chelsea wameshinda mechi sita za Premier League mfululizo bila ya kuruhusu goli hata moja, wamecheza dakika 590 tangu mara ya mwisho walipofungwa na Arsenal 3-0 kwenye Premier September 24.

Chelsea wamejikusanyia alama 15 kutokana na michezo yao sita ya nyumbani msimu huu. Alama nyingi zaidi kuliko timu yoyote.

Wamefunga mabao 18 na kuruhusu matatu kwenye michezo hiyo sita katika Uwanja wa Stamford Bridge.

Diego Costa ni mchezaji wa kwanza kwenye Premier League msimu huu kufikisha mabao 10 msimu huu. Amefunga mabao hayo ndani ya michezo 12.

Costa amehusika kwenye magoli mengi zaidi katika Premier League msimu huu kuliko mchezaji yeyote (amefunga mabao 10 na kutoa assists tatu)
Tottenham

Tottenham hawajafungwa ndani ya mechi zao 12 za Premier League walizocheza msimu huu (wameshinda mechi sita, droo sita).

Hata hivyo, ushindi wao dhidi ya West Ham wiki iliyopita ni ushindi pekee kwenye mechi tisa kwenye mashindano yote msimu huu (droo tano, kufungwa tatu).

Alama 24 walizonazo Spurs kwenye michezo 12 ni tatu zaidi ya walizokuwa nazo msimu uliopita katika hatua kama hii, licha kuwa katika nafasi ile ile ya tano.

Tangu kuanza kwa msimu uliopita, Spurs wamevuna alama 20 kwenye mechi za London derby kwenye Premier League. Pointi nyingi zaidi kuliko timu yoyote.

Kujua Mbinu Za Kumfikisha Kileleni Mwanamke Kwa Haraka: BONYZA HPA CHNI

Kujua Sehemu 10 Zinazompa Raha mwanamke wakati wa Tendo, BONYZA HAP 1UU
BOFYA LIKE KUUNGANA NASI FACEBOOK!During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip.
© Copyright Masama Blog | Designed By MASAMA TEAM
Back To Top