Ticker

10/recent/ticker-posts

Kumbe Pesa kwenye mahusiano ya kimapenzi ni muhimu ???...huyu Pesa anazo lakini hanihusishi nifanyeje?


Image result for mapenzi image
Pesa muhimu sana ktk maisha yetu, pesa ni sabuni ya roho (well mapenzi pia ukiyapata yale ya kweli), Pesa husababisha penzi kufa, kunawili, kukomaa, kukua n.k.

Haijalishi pesa inatoka wapi, iwe pande zote mbili au kwa ushirikiano as mnabiashara/Kampuni as family/pea a.k.a couple au inatoka upende mmoja as kwa mwanamke au mwanaume tu.

Hivi wewe na mpenzi wako huwa mnafanikiwa kujadili maswala ya uchumi (pesa) ndani ya uhusiano wenu bila vita? Well, I mean kuzozana?

Je mpenzi wako ni mbahili? unakabiliana vipi na ubahili wake?

Nakumbuka mama yangu alikua akifanya kazi na baba pia lakini walikuwa hawaishi kuzozana kuhusiana na matumizi yao ya pesa za ziada au niseme akiba (mara baada ya kutimiza mahitaji yote muhimu ndani ya nyumba, Baba alikuwa akizitumia kunywa na wafanyabiashara wenzake wakati mama alikuwa akizitumia zake za ziada kutoa “fungu la kumi” Kanisani.


Migogoro au mizozo kuhusu maswala ya uchumi nikiwa na maana pesa huchangia kwa kiasi kikubwa kuharibika kwa uhusiano wenu. Unatakiwa kujijua umesimama wapi kiuchumi ktk uhusiano wako, nikiwa na maana wewe tegemezi, kipato chako kidogo/kikubwa, kipato kizuri lakini bahili, vipato vyenu wote 2 haviwatoshelezi n.k


Ukitambua wapi ulipo kiuchumi hakikisha pia unajua tofauti ya haki na wajibu wako ktk uhusiano wenu (wengi huchanganya maana halisi ya haki na wajibu).

Mpenzi tegemezi-

Ili kuepuka mzozo wa jinsi gani unatumia pesa unazopewa kila siku ni vema basi ukajifunza kufanya manunuzi ya vitu chee (rahisi) na kinachobaki pale kitunze (weka akiba), kumbuka kuwa ili mpenzi afurahie chakula utakachokipika huitaji kutumia pesa nyingi kwa siku na badala yake ongeza ujuzi/utundu ktk mapishi yako….ni mfano tu unaweza ukawa unapewa laki au mia tano kama sio unaagizwa ukaombe chakula kwenu.

Ikiwa wewe mwanaume ndio mwenye kipato basi tambua kuwa ni wajibu wako kumhusisha na kushirikiana na mkeo/mpenzi ktk utengenezaji wa “bajeti” sio kwa vile unazileta basi mambo ya “bajeti” na maamuzi mengine ya kiuchumi unatoa wewe.


Kumbuka kuwa unapokuwa kwenye uhusiano mnafanya mambo yote kwa usawa na kuthaminiana sio kwa vile masikini (hana kipato) basi ndio hawezi hata kushauri au kutoa wazo kama sio uamuzi wa kufanya jambo Fulani n.k


Vipato vyenu havitoshelezi- 

Nafikiri unatambua kuwa maisha huwa hayabaki vilevile kila siku, maisha hubadilika na hivyo mtindo wetu wa kuishi hubadilika pia. Mfano nyote mlikuwa mkifanya kazi na mlikuwa “comfortable” na maisha yenu then mke/mpenzi anakuja kuzaa watoto 3 kwa mpigo au mmoja wenu anaachishwa kazi…huwezi kuishi kama mlivyokuwa mkiishi hapo awali, na hakika swala zima la uchumi linabadilika.


Hili likitokea wewe na mpenzi wako mnatakiwa kukubaliana kubadilisha aina ya maisha na kuishi kutokana na majukumu yaliyojitokeza wakati huo, kitu kitakacho wasaidia kuepuka mzozo kuhusu uchumi/pesa.


Mpenzi m-bahili-

“dizaini” hii ni ngumu sana kuishi nayo lakini kama kwa bahati mbaya umegundua wakati tayari ushaolewa/oa basi jifunze tu jinsi ya kukabiliana nae nakuongeza mapenzi yako juu yake.


Ili kuepuka mzozo kuhusu uchumi/pesa ni vema kugawana majukumu, yule mwenye kipato kikubwa basi anafanya yake makubwa na yule mwenye kipacho kidogo basi anafanya yale madogo na hakikisha mnakuwa na “account” moja kwa ajili ya maswala hayo bila shaka mtaishi raha mstarehe bila kuzozana kuhusu pesa.


Mpenzi mwenye kipato kidogo-

Jinsi ya kuepuka mzozo hakuna tofauti sana na hapo juu kwamba mwenye kikubwa afanye makubwa na mwenye kidogo afanye yale ya kawaida.