KUMBE HIZI NDIZO SABABU ZA RAY C KUTOPANDA JUKWAA LA FIESTA LEADERS CLUB | Masama Blog

KUMBE HIZI NDIZO SABABU ZA RAY C KUTOPANDA JUKWAA LA FIESTA LEADERS CLUB


Weekend iliyopita Dar es Salaam nzima kila kona story ilikuwa ni Fiesta tu, ambayo ilikuwa ndio kilele cha msimu huo wa burudani ambayo ilifanyika Dar es Salaam pande za Leaders Club.
Moja kati ya shows kali ambazo zilihappen usiku ule ni ile ya Mnako Lord Eyez, na shangwe lilikolea zaidi pale alipopandishwa mwanadada Nandy ili kuperform part ya mkongwe Ray C katika show hiyo.
Unachotakiwa kukifahamu ni kwamba Ray C mwenyewe ndiye ambaye alikuwa kapangwa ili kuweza kutisha pale stejini lakini kuna mambo flani ambayoo yalitokea na kusababisha mambo kushindwa kwenda jinsi yalivyo pangwa.
Nandy amepiga story na Amplifaya ya Clouds FM na kuweka wazi kuwa ni Ray C ambaye alikuwa amepangwa lakini mambo yalikwenda tofauti.
“Niliwish sana Ray C apande ili aweze kuimba ile part yake lakini kuna vitu ambavyo haviku kaa sawa ndio maana hakuweza kupanda. Me nawish sana Ray C aweze kurudi kama zamani kwenye game ya music, kwasababu bado naamini ana ile nafasi ya kukaa pale pale alipokuwepo zamani. Ni mtu mwenye kipaji, na anaweza kwasababu muziki wake unaishi.” Alisema mwanadada Nandy

Back To Top