ITEGEMEE COLLABO YA DIAMOND PLATNUMZ NA NEYO KUCHEZWA KWENYE VITUO VIKUBWA MAREKANI | Masama Blog


ITEGEMEE COLLABO YA DIAMOND PLATNUMZ NA NEYO KUCHEZWA KWENYE VITUO VIKUBWA MAREKANI


Imekuwa ni ngumu sana kwa ngoma za Afrika kupata airtime kwenye vituo vya TV & Radio vya Marekani hata kama ikiwa ni collabo ya msanii wa Africa na wa Marekani.
Lakini Diamond Platnumz ameituma Pe ifikishe ujumbe kwa mashabiki zake kuwa wasihofu juu ya hilo kutokana na uungwana ambao amefanyiwa na mkali wa Marekani ambaye kafanya nae Collabo Neyo.Diamond Platnumz amesema kuwa Neyo ni msanii ambaye ametokea kumkubali tu kiasi kwamba hakuweza kuleta kwere katika suala zima la kudondosha saini ili ngoma hiyo ipigwe katika
vituo vya nchini kwao. Kitu ambacho huwa ni ngumu sana kwa wasanii wanchini humo kufanya hivyo.“Kiukweli sielewi ni kwasababu gani, lakini katika nchi ambazo wanakaza miziki ya kiafrica isiingie kwao Marekani ni yakwanza. Yani wao wako radhi mfanye lakini wengi wanagoma kusaini nyimbo yako ipigwe nchini kwao. Namshukuru mwenyezi Mungu Neyo ni mtu ambaye naona katokea kunitunuku tu yani, nyimbo yangu kakubali ichezwe Marekani pamoja na watu wengi tu ninaofanya nao kazi, nahisi nina bahati tu. Lakini mara nyingi huwa wanakataa kusaini, wao huwa wanataka wenyewe tu ndio wapigwe huku lakini sisi tusipigwe kwao.” Alisema Diamond Platnumz
Play hii video hapa chini uweze kumsikiliza mwenyewe Diamond akiwa anafunguka juu ya suala hilo.

BOFYA LIKE KUUNGANA NASI FACEBOOK!


UNAIJUA BIASHARA YA FOREVER LIVING?....Kama una mtaji kuanzia 250,000 hadi 1,020,000 na unapenda kujikwamua na kubadilisha maisha yako kupitia biashara hii Tupigie simu nambari 0625539100 au 0625539200