IDADI YA WATU WALIOFARIKI KWENYE AJALI YA NOAH,LORI SHINYANGA YAFIKIA 19 | Masama Blog


IDADI YA WATU WALIOFARIKI KWENYE AJALI YA NOAH,LORI SHINYANGA YAFIKIA 19

Idadi ya watu waliopoteza maisha katika ajali ya gari ndogo Toyota Noah yenye namba za usajili T 232 BQR kugongana na lori aina ya Scania lenye namba za usajili T198CDQ na tela lake lenye namba T283CBG imefikia 19 baada ya majeruhi mmoja kufariki dunia. 
Kaimu mganga mfawidhi wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga Dkt. Daniel Maguja amesema majeruhi aliyefariki ni mtoto anayeitwa Hamisa Matiko Ali mwenye umri wa miaka mitano ambaye hali yake ilibadilika ghafla na kufariki majira ya saa mbili usiku jana Novemba 07,2016.
Mtoto huyo amefariki dunia wakati akiendelea kupatiwa matibabu katika hospitali hiyo. 
Mama mzazi wa mtoto huyo Debora Maingu alifariki dunia katika ajali hiyo. 
Majeruhi mwingine (mtoto) Salima Kiza mwenye umri wa mwaka mmoja ambaye alivunjika mfupa wa paja la kushoto alipewa rufaa ya kwenda kutibiwa hospitali ya rufaa ya Bugando jijini Mwanza na majeruhi Boniface Richard anaendelea kupatiwa matibabu hospitalini hapo.

BOFYA LIKE KUUNGANA NASI FACEBOOK!


UNAIJUA BIASHARA YA FOREVER LIVING?....Kama una mtaji kuanzia 250,000 hadi 1,020,000 na unapenda kujikwamua na kubadilisha maisha yako kupitia biashara hii Tupigie simu nambari 0625539100 au 0625539200