HUYU NDIYO MPENZI WA MSANII RAYVANNY WA WCB | Masama Blog


HUYU NDIYO MPENZI WA MSANII RAYVANNY WA WCB

rayx

Ule usemi wa Kiswahili unaosema ‘penzi ni kikohozi kulificha hauwezi’ unazidi kujidhihirisha kwa muimbaji wa WCB, Rayvanny baada ya anayedaiwa kuwa mpenzi wake kuonyesha ni jinsi gani anavyomzimia mkali huyo wa wimbo, Sugu.
Mwaka huu mwanzoni Rayvanny alipost picha mtandaoni akiongelea na mrembo huyo hali ambayo iliibua maswali mengi kutokana na picha hiyo kutoonyesha sura ya mrembo huyo.
yrat

Muimbaji huyo hakuwahi kuzungumza chochote kuhusu mrembo huyo, lakini binti huyo anayedaiwa kuwa ni mpenzi wake ameamua kufunguka kupitia mtandao wa instagram kuonyesha jinsi gani anampenda mkali huyo wa wimbo, ‘Natafuta kiki’.
“Nakupenda sana mumewangu hakuna wakufanana na wewe mm bado sijaona 💑,” aliandika instagram mrembo huyo huku akiwa amepost picha hapo chini.
ray-vanny
rayvanny


BOFYA LIKE KUUNGANA NASI FACEBOOK!


UNAIJUA BIASHARA YA FOREVER LIVING?....Kama una mtaji kuanzia 250,000 hadi 1,020,000 na unapenda kujikwamua na kubadilisha maisha yako kupitia biashara hii Tupigie simu nambari 0625539100 au 0625539200