HIZI NDIZO SABABU ZILIZOMFANYA WAZIRI MKUU WA DR CONGO KUJIUZULU MAPEMA LEO HII | Masama Blog


HIZI NDIZO SABABU ZILIZOMFANYA WAZIRI MKUU WA DR CONGO KUJIUZULU MAPEMA LEO HIIWAZIRI   mkuu nchini Jamhuri ya Demokrasi ya Congo Augustin Matata Ponyo, ameamua kujuuzulu mapema leo hii ili kuacha serikali ya mpito. 
Lakini pia amejuuzulu ili kutoa fursa kwa mrithi wake kuiongoza seriklai hiyo.

Kujiuzulu kwa bwana Ponyo ni sehemu ya makubaliano yaliyotiwa sahihi mwezi uliopita kati ya serikali ya Rais Joseph Kabila na baadhi ya vyama va upinzani ya kuhairisha uchaguzi wa urais hadi mwezi Aprili mwaka 2018.

Wapiga kura nchini DRC walistahii kupiga kura mwezi huu kumchagua mrithi wa Rais Kabila, wakati wa kumalizika kwa mhula wake wa mwisho.

Vyama vikuu vya upinzani vinakataa kuhairishwa kwa uchaguzi vikisema kuwa hiyo ni njama ya Rais Kabila ya kusalia madarakani.

Baraza lote la mawaziri lilijiuzulu na bwana Ponyo.
chanzo BBC Swahili

BOFYA LIKE KUUNGANA NASI FACEBOOK!


UNAIJUA BIASHARA YA FOREVER LIVING?....Kama una mtaji kuanzia 250,000 hadi 1,020,000 na unapenda kujikwamua na kubadilisha maisha yako kupitia biashara hii Tupigie simu nambari 0625539100 au 0625539200