Hii ndiyo Taarifa Kuhusu Kinachoendelea Kwenye Kesi ya Scorpion Mtoa Macho MahakamaniUpelelezi wa kesi inayomkabili Salum Njwete maarufu kama Scorpion anayetuhumiwa kumsababishia upofu wa kudumu Saidi Mrisho umekamilika na hatimaye shauri hilo litasomwa Novemba 30 mwaka huu katika mahakama ya manispaa ya Ilala.

Njwete anatarajiwa kusomewa mashtaka yake baada ya yale ya kwanza kufutwa ambapo itakuwa ni mara ya kwanza kusikilizwa baada ya kufunguliwa mashtaka mapya.

Huyu ndiye Scropion, kijana aliyejizolea umaarufu ambapo watu wengi hupenda kumshuhudia kila aingiapo na kutoka mahakamani huku kila mmoja akizungumza lake kwa kesi inayomkabili.

Alipoingia mahakamani leo, aliomba ufafanuzi wa wazi juu ya mashtaka yanayomkabili ambapo upande wa jamhuri kupitia kwa wakili wake Chesensi Gavyole walisema ushahidi umekamilika.

Kutokana na kuombwa ufafanuzi, Hakimu anayesimamia kesi hiyo Flora Haule amesema baada ya upelelezi huo kukamilika kesi hiyo itasomwa Novemba 30 mwaka huu, hivyo mshtakiwa atapata ufafanuzi wa mashtaka yake .

Ikumbukwe kwamba Oktoba 19 mwaka huu, Salum Njwete maarufu kama Scropion alifutiwa kesi na kisha kusomewa upya mashtaka yake kutokana na uamuzi wa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) aliyeomba kufanya hivyo baada ya hati ya awali kuwa na mapungufu ya kisheria

Kujua Mbinu Za Kumfikisha Kileleni Mwanamke Kwa Haraka: BONYZA HPA CHNI

Kujua Sehemu 10 Zinazompa Raha mwanamke wakati wa Tendo, BONYZA HAP 1UU
BOFYA LIKE KUUNGANA NASI FACEBOOK!During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip.
© Copyright Masama Blog | Designed By MASAMA TEAM
Back To Top