Mtandao maarufu wa Habari za Burudani nchini Nigeria umetoa List ya wasanii waliofanya vizuri kwa mwaka 2016. Hii sio mara yake ya kwanza kwa Mtandao huo kutoa list, bali huo ndio utaratibu wao kila mwisho wa mwaka kutoa list ya wasanii waliofanya vizuri Nchini humo.
Utoaji wa list hiyo kila Mwaka ulianza mnamo mwaka 2011 na kuendelea mpaka sasa. Kila list ya kila mwaka huwa Mtandao huo una ruhusu pia wadau wachangie maoni yao na kupendekeza majina Kabla list haijatolewa rasmi.
Vigezo vya kuweka list hiyo ni pamoja na
kuzingatia utoaji wa wimbo/Nyimbo kali kwa mwaka husika, Idadi ya show za ndani na nje ya Nchi, Matangazo, Dili za mikataba na Lebo kubwa za muziki, Kukua kwa msanii kutoka wa kitaifa hadi kimataifa.
Kwa vigezo hivyo hii ndiyo Orodha ya Majina 10 ya wasanii wa muziki waliofanya vizuri nchini Nigeria kwa Mwaka 2016 na Takwimu zilizofanywa na mtandao wa NotjustOK.

1. Wizkid

2. Tekno

3. Olamide

4. Phyno

5. Kiss Daniel

6. Falz

7. Adekunle Gold

8. Mr Eazi

9. Reekado Banks

10. Davido
Hata hivyo maswali yalikuwa mengi kwa wasanii ambao wana majina makubwa lakini hawaja orodheshwa kwenye list hiyo wakiwemo Tiwa Savage, Patoranking, Timaya, Yemi Alade na Lil Kesh jibu ni kwamba hao wamefanya vizuri zaidi nje ya Nigeria na Hata nyimbo zao hazijavuma kwenye media za Nigeria.

BOFYA LIKE KUUNGANA NASI FACEBOOK!


Je wewe una mtaji wa Ths.250,000/= au 510,000 au 1,020,000?..na unahitaji kufanya biashara kubwa kwa mtaji huo ufanikiwe?..basi kama ndiyo njoo tukuonyesha njia ya kutekeleza malengo yako...piga 0625 539 100

 
Top