HANSCANA AFUNGUKA KUHUSU WASANII WA BONGO KURUDIA NA KUFANANA KWA VIDEO ZAO | Masama Blog


HANSCANA AFUNGUKA KUHUSU WASANII WA BONGO KURUDIA NA KUFANANA KWA VIDEO ZAO

Muongozaji wa video na mshindi wa Tuzo za Watu 2015, Hanscana ambae pia ametisha sana kwenye utengenezaji wa video mpya ‘Muziki’ ya Darasa, pia ndiye director anayekuja kwa kasi kutokana na ubora wa kazi zake.

Muongozaji huyo na mtayarishaji wa video nchini Hanscana, amesema sababu inayo pelekea video nyingi za bongo kurudiwa na kufanana ni kutokana na maamuzi na mapendekezo ya msanii mwenyewe anacho pendelea.
hanscana4
Hanscana
Akipiga story ndani ya eNewz amesema “Ukiona kuna kitu kimerudiwa katika video ujue kuna makubaliano kati ya muongozaji na msanii kwa kuwa mara nyingi msanii anapo andika wimbo wake anakuwa na wazo la aina ya video ambayo anaitaka hivyo wasanii ni kama wateja wetu na tunafanya anachokitaka mteja wetu”.
Pia Hanscana amesema kwamba yeye na Khalfani ni marafiki japo hawajawahi kufungua kampuni moja ila wakati wanatafuta maisha waliwahi kuishi nyumba moja kwa sasa kinacho watenganisha ni kutokana na kila mmoja kuzidi kutafuta maisha yake japo bado ni marafiki.

SHARE


BOFYA LIKE KUUNGANA NASI FACEBOOK!


UNAIJUA BIASHARA YA FOREVER LIVING?....Kama una mtaji kuanzia 250,000 hadi 1,020,000 na unapenda kujikwamua na kubadilisha maisha yako kupitia biashara hii Tupigie simu nambari 0625539100 au 0625539200