Kutengeneza uhusiano wenye nguvu ni moja ya mambo yenye changamoto kubwa. Japo hakuna maelekezo maalum, kuna mambo machache na rahisi ambayo unaweza kumwambia mpenzi wako yakaujenga zaidi. Weka desturi ya kusema mambo haya kwa mpenzi wako na muda mfupi tu mtakuwa couple itakayowapa wivu marafiki zetu.
1. Nakupenda: Ni kitu rahisi na cha wazi cha kumwambia mpenzi wako. Hakikisha tu kuwa unamaanisha. Jaribu kulisema neno hilo pindi mpenzi wako anapokuchekesha au pale anapofanya kitu kinachokukumbusha kwanini mko pamoja.
2. Nilikuwa nakuwaza: Ni muhimu kumjulisha mpenzi wako kuwa unamuwaza hata kama hamko sehemu moja.Ukiona kitu kizuri au cha kuchekesha katika siku yako ambacho kinakufanya umkumbuke, mjulishe.
3. Siku yako ilikuaje?: Muulize masuala ambayo mpenzi wako anakutana nayo katika shughuli za kila siku. Muulize kuhusu huyo mfanyakazi mwenzie anayemkera au kazi kubwa waliyokuwa wakifanya. Kumpa nafasi mpenzi wako kushare sehemu zingine za maisha yake kutasaidia kuunganisha dots kati ya muda mnaokuwa pamoja.
4. Unga mkono maamuzi mazuri ya mpenzi wako: Mpe moyo mpenzi wako kwa kumjulisha kuwa unaunga mkono maamuzi yake. Unaweza ukaenda mbali zaidi kwa kujaribu kumsaidia afanikishe malengo aliyojiwekea.
Maisha yamejaa vikwazo vingi, na ile hisia kuwa una mtu mwingineupande wako zinaweza kukusaidia kuvivuka. Msiwe couple tu, kuweni timu. Kumkumbusha mpenzi wako kuwa upo nyuma yake kutaimarisha uhusiano wenu.
5. Mwambie mpenzi wako kuwa Umependeza: Kama umekuwa kwenye uhusiano kwa muda mrefu, ni rahisi kujisahau katika mengi. Ni muhimu kumkumbusha mpenzi wako kuwa anakuvutia. Kumjulisha kuwa ‘gauni hilo limekupendeza sana’ kutamfanya ajisikie vizuri na kukumbusha kwanini ulimchagua yeye. 
6. Samahani ni neno zuri kwa mpenzi wako: Kila mtu hukosea wakati fulani. Wakati mwingine hujikuta tukiongea maneno kwa hasira na baadaye kugundua kuwa hatukuwa sahihi. Ubishi hauna nafasi kwenye uhusiano wenye furaha, hivyo omba msamaha unapofanya kosa. Omba msamaha kwa kukasirika. Omba msamaha kwa kuumiza hisia za mpenzi wako. Omba msamaha hata kwa vitu ambavyo sio kosa lako.
7. Hakuna kama wewe: Mpenzi wako anatakiwa kuwa rafiki yako. Kama hautaki kutembea naye, basi hamkupaswa kuwa kwenye uhusiano. Mfanye mpenzi wako ajue kuwa yeye ni bora na hakuna kama yeye.

8. Napenda mawazo yako Picha: StudioMwambie mpenzi wako kuwa unapenda mawazo yake. Mjulishe kuwa unaona anaakili, mcheshi, anajua kupenda na ana kipaji.
9. NakuheshimuKama ulivyo uhusiano wa marafiki, heshima ni kitu muhimu kwako na mpenzi wako. Mpe nafasi ya kukushauri au kukupa mawazo kwenye mambo yanayokutatiza. Mtu anapohisi anaheshimiwa, hujisikia pia furaha na salama, vitu ambavyo ni muhimu kwenye uhusiano wowote mzuri.
10. Napingana na hilo: Sehemu moja wapo ya kumheshimu mpenzi wako ni kumjulisha pale usipokubaliana naye. Hakuna mtu anapenda kuoa mtu anayekubaliana na kila kitu na hakuna mwanamke anayetakakuzaa watoto na mwanaume asiye na msimamo. Mnaweza kuwa timu, lakini nguvu ya timu yoyote ipo kwenye mawazo na matendo ya kila mmoja.
Kuwa na maoni yako na yaseme kwa mtindo wa heshima. Kumpa mpenzi wakomtazamo tofauti kunaweza kumsaidia kupata suluhisho kwa tatizo ambalo hakuwa ameliwaza.11. Usiku mwemaTunaishi kwenye wakati ambapo mawasiliano ni rahisi mno.BOFYA LIKE KUUNGANA NASI FACEBOOK!


Je wewe una mtaji wa Ths.250,000/= au 510,000 au 1,020,000?..na unahitaji kufanya biashara kubwa kwa mtaji huo ufanikiwe?..basi kama ndiyo njoo tukuonyesha njia ya kutekeleza malengo yako...piga 0625 539 100

 
Top