Diamond Aelezea Sababu ya Kujiita Jina la Diamond PlatnumzDiamond Platnumz ni mmoja wa wasanii wakubwa barani Afrika kwa sasa. Siku za hivi karibuni alipata nafasi ya kushiriki tamasha la muziki la Coke Studio Afrika kusini ambapo alitengeneza wimbo uliowavutia wengi kwa kushirikiana na Cassper Nyovest, wimbo unaitwa My Heart.

Akiwa katika tamasha hilo alifanya mahojiano na waandaaji na moja ya yaliyowavutia wengie ni alipoeleza jinsi alipopata jina lake la sanaa ‘Diamond Platnumz.’

Akielezea chanzo cha jina hilo, Naseeb Abdul Juma alisema kuwa jina hilo lilianza kitambo alipokuwa akiimba ambapo rafiki zake mtaani walikuwa wakimwambia kuwa yeye ana kipaji kizuri cha kuimba na siku akipata mtu wa kukiendeleza, ataweza kuwa mwenye thamani kama Diamond.

Alieleza kuwa katika kipindi hicho walianza kumuita jina hilo la Diamond na kwavile hapakuwepo na msanii yeyote anayetumia jina hilo, akawaza kwanini asilitumie. Ndipo na yeye akaaza kujiita Diamond.

Akifafanua lilipotekea jina Platnumz, Naseeb alisema kuwa neno hilo lina maanisha mtu mtanashati mwenye swaga, mwenye muonekano wa kuvutia na mtu wakupendeza kila mara. Hivyo akajiita Diamond Platnumz na ukawa ndio mwanzo wa jina lake hilo.

Msikilize Naseeb Abdul Juma akielezea hapa chini. Vipande vingine vya mahojiano aliyofanya ameviweka kwenye ukurasa wake wa Instagram. 

Kujua Mbinu Za Kumfikisha Kileleni Mwanamke Kwa Haraka: BONYZA HPA CHNI

Kujua Sehemu 10 Zinazompa Raha mwanamke wakati wa Tendo, BONYZA HAP 1UU
BOFYA LIKE KUUNGANA NASI FACEBOOK!During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip.
© Copyright Masama Blog | Designed By MASAMA TEAM
Back To Top