Jeshi la polisi mkoani Mtwara linamtafuta mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Saidi Hamisi Kombo dereva wa gari yenye namba za usajili T 954 na tela lake yenye.no 397CCY aina ya Scania kwa kosa la kutoroka na shehena ya korosho magunia 405 yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni mia moja na 22 mali ya kampuni ya Starnuts Company Limited.
Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa polisi mkoa wa Mtwara Thobias Sedoyeka amesema tukio hilo limetokea eneo la maghalani kata ya Malopokelpo wilaya Tandaimba mkoani Mtwara.

Amesema dereva huyo alikabidhiwa magunia hayo ili kuyasafirisha kwenda bandari ya Mtwara lakini mtuhumiwa huyo alitoweka mara  tu baada ya kuingia mtwara mjini.

Hata hivyo amesema uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa namba za gari  alizotumia mtuhumiwa ni bandia kwani namba hizo ni za gari aina ya Isuzu Carry na namba halisi za gari hilo ni T 852 APL na tela lake ni T 198 AKY mali ya Gulled Transport LTD inayomilikiwa na Abdi Hers wote wakiwa wakazi wa Dar es Salaam.

Kamanda amesema juhudi za kumtafuta zinaendelea na kutoa wito kwa wakazi wa Mtwara kuwa makini na wezi na matapeli hasa kipindi hiki cha mwisho wa mwaka ambapo vitendo vya hali hiyo vimekuwa vikiongezeka.

BOFYA LIKE KUUNGANA NASI FACEBOOK!


Je wewe una mtaji wa Ths.250,000/= au 510,000 au 1,020,000?..na unahitaji kufanya biashara kubwa kwa mtaji huo ufanikiwe?..basi kama ndiyo njoo tukuonyesha njia ya kutekeleza malengo yako...piga 0625 539 100

 
Top