Mahakama ya Wilaya Kinondoni imemtia hatiani mwanamuziki nguli wa Bongo Fleva, Judith Wambura “Lady Jaydee” (pichani juu) kwa kutoa maneno ya kashfa dhidi ya viongozi wa Clouds Media Group Joseph Kusaga na Ruge Mutahaba.Mahakama hiyo imemuamuru aombe radhi kupitia kwenye chombo cha habari chenye “coverage” kubwa nchini kote na ikiwezekana duniani.

Joseph Kusaga.
Katika kesi hiyo, Jaydee anashtakiwa na viongozi wa Clouds Media Group ambao ni Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Joseph Kusaga na Mkurugenzi wa Utafiti wa Redio hiyo, Ruge Mutahaba kwa kuuchafua uongozi wa kampuni hiyo na viongozi wake kupitia mitandao ya kijamii katika malumbano makali kati ya pande hizo mbili.

Ruge Mutahaba.
Mei 2013, Clouds Media Group na Ruge walimburuza Jaydee mahakamani kwa kile walichodai kwamba alikuwa akiwatukana kwenye mitandao ya kijamii.
BOFYA LIKE KUUNGANA NASI FACEBOOK!


Je wewe una mtaji wa Ths.250,000/= au 510,000 au 1,020,000?..na unahitaji kufanya biashara kubwa kwa mtaji huo ufanikiwe?..basi kama ndiyo njoo tukuonyesha njia ya kutekeleza malengo yako...piga 0625 539 100

 
Top