ALI KIBA AFUNGUKA KUHUSU KUWA NA LEBO! JOKATE NA ABBY SKILLS WATAJWA KUWA CHINI YA LEBO HIYO. | Masama Blog


ALI KIBA AFUNGUKA KUHUSU KUWA NA LEBO! JOKATE NA ABBY SKILLS WATAJWA KUWA CHINI YA LEBO HIYO.

Imekuwa ni kama fashion sasa kwa wasanii wa Bongo Fleva kwa kila mmoja kutaka kuwa na lebo yake, ukiachilia mbali wale ambao walikwisha tangulia kwenye mambo hayo na lebo zao zikafanya poa.Sasa mkali wa Bongo Fleva Alikiba ameichana Pe kuwa kuhusu suala la Lebo yeye ameshawahi kuwa nayo kitambo, na kuna wasanii ambao alikuwa akiwasimamia lakini kwa muda fulani alikuwa amepumzika kidogo juu ya jambo hilo.
King Kiba ameitobolea siri kuwa yuko katika maandalizi ya kurudi rasmi katika suala hilo la kusimamia wasanii (Kuanzisha Lebo) na tayari kuna wasanii ambao amekwisha fanya nao mazungumzo na watakuwepo chini ya lebo hiyo.
“Me record lebo ninayo muda mrefu, lakini sikuifanya matangazo, lakini kuna wasanii ambao nilikuwa nawamiliki nikapumzika, sasa hivi narudi tena najipanga upya kama unavyomuona Abby Skills anafanya kazi vizuri na bado ataendelea kufanya kazi zingine, Abdu Kiba pia ametoa ngoma hivi karibuni lakini haijafanya vizuri lakini ngoma ijayo itakuwa ni ya mimi na yeye. Pia kuna msanii mwingine ambaye watu hawajawahi kumsikia, pia kuna wakina Jokate, kina Dalila na wengine kibao tu ambao wapo chini ya Lebo yangu.”
Hayo ni baadhi tu ya maneno ambayo Alikiba alibonga na . Kusikiliza full interview play hii video hapa chini.

BOFYA LIKE KUUNGANA NASI FACEBOOK!


UNAIJUA BIASHARA YA FOREVER LIVING?....Kama una mtaji kuanzia 250,000 hadi 1,020,000 na unapenda kujikwamua na kubadilisha maisha yako kupitia biashara hii Tupigie simu nambari 0625539100 au 0625539200