Ahadi ni deni – muigizaji mkongwe wa Marekani, Samuel L. Jackson ameonekana kuipinga ahadi yake aliyowahi kuitoa kuwa atahamia Afrika Kusini endapo Donald Trump atateuliwa kuwa Rais wa nchi hiyo.

Kupitia mitandao yake ya kijamii, Jackson aliandika, “If that motherf- -ker becomes president, I will move my black ass to South Africa.”

Hatimaye muigizaji huyo amekuja na ujumbe mpya kupitia mtandao wake wa Twitter, ameandika, “Why y’all so anxious for me to leave?! I pay More Taxes than All U Trumpafukkaz… Him too!!.”

Trump alichaguliwa kuwa Rais wa Marekani Jumatano ya Novemba 9, kwa kushinda majimbo ya uchaguzi 276 huku Clinton akishinda 218.

TOA MAONI YAKO HAPA

 
Top