Wanawake wanaotumia kope bandia wanahofiwa kuwa na
hali ya hatari ya kupata upofu wa macho kutokana na gundi
wanazotumiwa kutumia kope hizo kuripotiwa kuripotiwa
kuwa na athari kwenye macho yao.
Tahadhari hiyo imetolewa na mratibu wa huduma ya macho
ya mkoa wa Iringa, Dk George Kabona,alipokuwa akitoa
tathmini ya huduma ya macho ikiwa ni sehemu ya kuelekea
maadhimisho ya siku ya afya ya macho duniani.
“Ningependelea wasipende kuzivaa kama fasheni ya
kawaida,kwasababu zina madhara sana. Kwasababu hizo
kope unabandika kwa kile kitu ambacho ile chemical ya
kubandikia ndio huwa inaogopwa zaidi kuliko hata kope
zenyewe. Ingekuwa labda unazibana na stapler hivi labda
lakini kuna kitu unabandikia ile kitu ndio jicho halikitaki
kama kinaendelea kukaa pale muda mrefu,”alisema Kabona.

TOA MAONI YAKO HAPA

 
Top