Ikiwa zimepita wiki kadhaa tangu tetemeko la ardhi litokee Kagera, leo October 6 2016 kupitia kituo cha runinga cha ITV kimeripoti habari kutokea hukohuko Kagera ambapo wananchi wa bonde la Katarabuga wamepatwa na taharuki baada ya kuibuka moto ardhini wakidhani volcano. Wakala wa jiolojia, Prof Mruma amesema moto huo ni wa kawaida tu hivyo wananchi wasiwe na taharuki yoyote, Prof. Mruma amesema…….
>>>’Huu moto unaunguza ardhi ambayo umejaa vipandevipande vya miti mikavu majani, mizizi mithili ya mtu anayetengeneza mkaa’
>>>’Volcano haiwezekani hapa, volcano ni uji wa miamba na ya chini kabisa ya volcano degree 400 kwa hiyo degree 400 centigrade ikiungua hapa hata huu mti usingesalia, volcano mara nyingi inatoka na majimaji na mvuke’
>>>’huu ni moto wa kawaida, moto kama huu unatokea kwenye ardhi ambayo ina uozo wa majani mengi sasa yale majani yakiungua yanatoa kitu kama hiki, moto wa namna hii mara nyingi inatokea kwenye makaa ya mawe mtu anapita anaangusha moto mkaa unalipuka panaanza kuungua na ardhi inachubukachubuka hivihivi’

BOFYA LIKE KUUNGANA NASI FACEBOOK!


Je wewe una mtaji wa Ths.250,000/= au 510,000 au 1,020,000?..na unahitaji kufanya biashara kubwa kwa mtaji huo ufanikiwe?..basi kama ndiyo njoo tukuonyesha njia ya kutekeleza malengo yako...piga 0625 539 100

 
Top