VIDEO:Kauli ya Ya Mama Lwakatare imemgusa Mrema, kapendekeza haya kwa Makanisa na Misikiti | Masama Blog


VIDEO:Kauli ya Ya Mama Lwakatare imemgusa Mrema, kapendekeza haya kwa Makanisa na Misikiti

Ni wiki imepita kwa mchungaji wa kanisa la mlima wa moto Assemblies of God , Mikocheni ‘B’ Dr. Getrude Lwakatare kutoa milioni 25 kuwalipia wafungwa ambao walikosa fedha kulipia faini na kufungwa jela.
September 15 2016 mwenyekiti wa bodi ya Parole Taifa Augustino Mrema amependekeza kufanyika kwa harambee kwa makanisa yote Tanzania.
Mrema ameomba makanisa yote kutoa sadaka ya siku moja ya Jumapili ili ikatumike kuwalipia faini wafungwa waliopo magerezani pia zoezi hilo lifanywe na Misikiti ikiwezekana.
Mrema ameomba hili zoezi lifanyike kabla ya sikukuu ya Christmas na mwaka mpya ili wafungwa waweze kusheherekea sikukuu hizo na familia zao lakini pia anataka wafanyabiashara, wenye viwanda na wakulima wakubwa nao wachangie kwenye kampeni hiyo ya kuwakomboa wafungwa kutoka magerezani.

ULIKOSA HII SABABU ZA MREMA KUAMUA KWENDA KUMUONA RAIS MAGUFULI? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI

BOFYA LIKE KUUNGANA NASI FACEBOOK!


UNAIJUA BIASHARA YA FOREVER LIVING?....Kama una mtaji kuanzia 250,000 hadi 1,020,000 na unapenda kujikwamua na kubadilisha maisha yako kupitia biashara hii Tupigie simu nambari 0625539100 au 0625539200