Image result for shiloleWiki iliyopita mwanadada Shilole aliachia video ya ngoma yake ya “Mtoto Mdogo Mdogo” ambayo kafanya na mkali wa Singeli Man Fongo.

Katika video hiyo matarajio ya wengi yalikuwa ni kumuona mwanadada Shilole akijiachia na kashkaji kadogodogo kama ngoma hiyo ilivyokuwa ikizungumza. Lakini cha kushangaza ni pale baada ya chupa hilo kutoka na kuonekana Shilole akikomelea kwa Dingilii flani hivi mwenye midevu yake (Mzee Chilo) tofauti na ilivyokuwa katika mawazo ya wengi.

Sasa Shilole amepiga story na Pe na kutuchana ni vipi alifikiria kubadilisha Idea ya video na kufanikiwa kuwashangaza wengi.
“Imekuwa kama surprise kwa watu wengi kwa mimi kumuweka Mzee Chilo wakati wao walitegemea mimi ntamuweka kijana under 18. Watanzania tunaishi sana kwa kukarili, mapenzi huwa hayachagui, mtu yeyote anaruhusiwa kumpenda yeyote yule ambaye kavutiwa naye, kama mimi nilivyodata kwa Mzee Chilo kwenye kichupa kile, idea ilikuja tu na nikaamua kufanya tofauti na watu walivyokuwa wakifikiria na kuonekana mimi namzimia sana Mzee kuliko kijana. Tuache kuishi kwa kukarili.” AlisemaShilole.
Ni mengi ambayo mwanadada Shilole alifunguka kuhusiana na ishu hiyo. Tazama hii video hapa chini kumsikiliza.
BOFYA LIKE KUUNGANA NASI FACEBOOK!


Je wewe una mtaji wa Ths.250,000/= au 510,000 au 1,020,000?..na unahitaji kufanya biashara kubwa kwa mtaji huo ufanikiwe?..basi kama ndiyo njoo tukuonyesha njia ya kutekeleza malengo yako...piga 0625 539 100

 
Top